Anapaswa kupeleka kwanza maombi ya kuomba kuwasilisha rufaa yake nje ya muda, rufaa hiyo isikilizwe kwanza kisha ikiwa mahakama itaona sababu zake ni za msingi itamruhusu kuwasilisha rufaa hiyo. Ikiona sababu zake hazijitoshelezi basi itatupilia mbali maombi hayo na hataweza tena kukata rufaa.