Anaswa akila nyama ya mtu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
11th August 2009


Katika kile kinachoonekana kuwa ni maajabu ya aina yake kutokea Bongo, mtu mmoja amenaswa na polisi na kisha kuswekwa mbaroni baada ya kudaiwa kukutwa akila nyama ya binadamu.

Mtu huyo, ambaye amedaiwa kukutwa akila nyama ya mwanadamu na huku akiwa na viungo kama sikio, viganja na kiungo cha uzazi cha mwanaume, ametambuliwa kwa jina la Zacharia Andrew, mkazi wa Kijiji cha Kakese wilayani Mpanda.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Jacob Mwarunda, ameiambia Alasiri kuwa Andrew alikutwa na viungo hivyo vya binadamu na anatarajiwa kuburuzwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa ili akabiliane na mashtaka ya mauaji.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda Mwarunda, mtu huyo alikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akisimulia zaidi, Kaimu Kamanda huyo akasema kuwa kabla ya kumnasa Andrew na viungo vya binadamu, kulikuwa na taarifa za mwili wa mtu kuokotwa porini.

“Julai 31 mwaka huu, mwili wa mtu uliokotwa Mpanda, eneo moja la pori ukiwa hauna baadhi ya viungo kama mikono na masikio... askari wa upelelezi walipofuatilia, ndipo wakapata taarifa zilizowezesha kukamatwa kwa mtuhumiwa akiwa na baadhi ya viungo vinavydhaniwa kuwa ni vya mwili wa mtu uliokutwa porini,” akasema Kaimu Kamanda Mwarunda.

Awali, kabla ya taarifa hizo rasmi za polisi kuthibitisha juu ya tukio hilo, baadhi ya wakazi wa eneo alikonaswa mtuhumiwa walikaririwa wakisema kuwa huwa anakula nyama za watu kwa vile eti ni tamu na kwamba si ya gharama kwa vile huwa haihitaji kuandaliwa na nakshi za viungo kama ilivyo kwa nyama nyingine.
http://www.ippmedia.com/
 
Mama yangu tunaelekea wapi jamni mbona inatisha hii?? au kala kwa imani za kishirikina?? mhh
 
mtu au binadamu ni mnyama kama wanyama wengine, kama ambavyo hatuoni taabu kula nyama ya ng'ombe, mbuzi, kima, fisi n.k basi tusione taabu inapotokea binadamu kamla binadamu mwenzie, sema tu haileti picha nzuri ukizingatia kuwa ni binadamu mwenzio otherwise to me its OK kula nyama ya mtu alimradi roho ya mlaji iridhie na kama itapatikana kwa urahisi why not??
 
Back
Top Bottom