Claret ameandika vyema sana. Nami nimalizie kwa mifano;
Mfano 1: Kaka yangu kabla hajaoa alikuwa na rafiki wa kike waliyependana sana kwa takribani mwaka mmoja. Aliamini binti alikuwa akimpenda lakini kuna jambo moyoni mwake lilimnyima amani juu ya huyo binti na hata alipoliwasilisha kwake walishindwa kukubaliana. Baada ya tafakuri na maumivu mengi alifanya maamuzi magumu ya kumaliza uhusiano ule kwa kuamini kila mmoja alistahili kuwa na amani kwenye uhusiano. Hakuwa binti mbaya, hakumkosea chochote.
alijisemea moyoni, atajipa muda akae peke yake na binti akae peke yake kila mmoja ajitafakari. Ikitokea akampata binti mwingine vyema, ataendelea na maisha. Ikitokea baada ya mwaka mmoja atakuwa peke yake, basi atamtafuta yule dada. Miezi tisa baadaye walikutana na katika kuongea hakuna hata mmoja wao aliyekuwa amedate mwingine (at least kwa kaka yangu ilikuwa hivyo). Wakazungumza na kugundua kumbe binti alishabadili kile walichokuwa wameshindwana mwanzoni. akaomba msamaha, akatangaza nia na juzi December walijaliwa mtoto wao wa pili.
Mfano wa 2: Kuna mzee mmoja kanisani ninapoenda alikuwa ameoa mke wake. Baada ya kutokuelewana katika ndoa yao kwa muda mrefu wakaachana. Kila mmoja akaenda kwa mwingine na kila mmoja akapata mtoto huko. Baada ya miaka 30, wamerudiana na kuoana tena. Wanatuaminisha wana furaha lakini kila nikienda kwao naona misuguano hasa kutoka kwa huyu mama. Hampendi mtoto wa huyo baba. Naona kama wanavumiliana tu.
Mfano wa 3: Nilimpenda binti. Akaniacha. Baada ya miezi akarudi. Nikampokea. Akaniacha tena. Alirudi baada ya miezi sita hivi akitaka kurudi. Katika kumuuliza akaniambia alikuwa kwenye uhusiano mwingine (uliofanya aniache) ila ameona ananipenda, ni tamaa na umbali kati yetu vilichangia. Nikasema asante nashukuru ila sina nafasi tena. Na huyu alijua nilikuwa ninampenda.
Niilikumbuka wimbo wa Crystal Gayle - Why have You Left the One You Left Me For.
Kwa ufupi, hakuna sheria kwenye mahusiano. Lakini kama unaamini haukuandikiwa mtu mmoja tu, basi piga moyo konde usonge mbele. Kama unaamini anaweza kuwa exception basi ushauri wangu ni muanze moja...kama marafiki, bila ahadi zozote. Usiwe na haraka maana najua una hisia naye bado, wewe ndo utakayeumia zaidi. Hakuna rafiki mzuri kama muda!
Kila la kheri mdogo wangu..usisahau kumuuliza kwanini amemuacha aliyekuacha kwa ajili yako!