Ananitangaza natembea na Mkewe

msemakweli2

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2013
Posts
1,627
Reaction score
1,886
Urafiki ni kazi sana, yupo mshikaji wangu mmoja anazunguka kwa marafiki ananitangazia eti natembea na mkewe. Kisa ni kwamba siku moja nilipita nyumbani kwake sikumkuta nikamkuta mkewe akanikaribisha nikawa namsubiri, shemeji mara akaniletea ubwabwa na juice nikawa nakula.

Baada ya muda nikamwambia shemeji naomba kwenda kubwaga haja ndogo chooni wakati natoka choo cha public ndani mara na shemeji akawa anatokea jikoni kwahiyo tukawa tumeongozana mimi mbele shemeji anakuja kwa nyuma, mara mlango wa koridoni ukafunguka jamaa ndio anarudi kwahiyo na sisi tumeongozana na shemeji nikaona kama kashtuka lakini alijikaza kiume.

Tukasalimiana na stori kidogo ila hakuniambia chochote kuhusu anachowaambia wengine, sasa ni mtu wa nne nakutana naye ananiambia jamaa anasema una mla mke wake, ninachoshangaa haniambii chochote tukikutana tunapiga stori tu

Sasa najiuliza huyu jamaa nimfanyeje nimuulize au niendelee kumuacha atangaze
 
Kosa langu mimi liko wapi?
Jr[emoji769]
 
Muulize

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utalogwa[emoji23]
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…