Ananipenda lakini simuhitaji

Acha ufala hiyo sio sifa, tumia busara na usijione upo juu.***** mmoja wewe.halafu jaribu kuvuta na picha umpende Demu halafu nae hakupendi name ukatangaze kwa watu
 
Test mzigo kama unafaa kwa matumizi ya binadamu jisogeze ila uwe na akili kubwa otherwise utanyanyasika mbele ya safari, mapenzi hiwa hayadumu ni tukio la muda mchache kama mwezi kupatwa na jua au jua kupatwa na mwezi, bada ya hapo huwa ni mazoea tu na kujitahidi kuwa pamoja.

Narudia tena kama anafaa jitahidi umpende tu. Siku nyingine usije rudi hapa umepata demu wa uswasi kwa mizinga mpaka unasingizia umekufa.
 
Kupo kupenda kwa aina 2 tu,kupo kupenda wewe mwenyewe,na kupo kupenda kwa kutengeneza,mfano wapo waliochaguliwa mke/mme na wazazi,lakini wanaendelea tu vizuri. Huyo binti mtunuku upendo wako na hakikisha upendo wako kweli umeuhamishia kwake kitu ambacho kinawezekana. Hakuna raha kubwa kama kupendwa wewe na mwanamke. Mchukukue jumla
 
Tatizo sio kukataa wito, kama miaka mitatu iliyopita nilipata dharau ya mwaka kutoka kwa mmoja wa hawa mageti kali hali iliyosababisha nichukie mabinti wote waliotoka katika hizi familia za kitajiri
 
Tatizo sio kukataa wito, kama miaka mitatu iliyopita nilipata dharau ya mwaka kutoka kwa mmoja wa hawa mageti kali hali iliyosababisha nichukie mabinti wote waliotoka katika hizi familia za kitajiri
Basi labda toka kipindi hicho umejijengea hofu kwa hao mabinti wa geti kali ndo maana unakosa hata hisia nae.
 
Mkuu oa mwanamke aliyekupenda, atakuvumilia kwa hali na shida, suala la huvutiwi nae ni la hisia tu unaweza kuelekeza moyo kwake ukaanza kuunda upendo kwake pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usimpotezee mda mkuu kama humpendi mwache atafute wakumpenda ucje msababishia heartbroken Dada wa watu bure
 
HUMPENDI HALAFU UNAOMBA USHAURI WA NINI ETI UMGANDE AU..YANI UNATAKA UMLIE TU PESA..BAADAE UWE NA MWINGINE MTOTO WA WATU APATE PRESHA AZIMIE...MAANA KWA MATENDO YAKE KAMA SIO MTOTO KIAKILI BASI KAKOLEA
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…