Wakati mwingine kuna haja ya kutulia uli umri ukisogea mambo mengine yatajifunua yenyewe....
Kuna tabia za kimsingi za wanawake ambazo ni nadra sana kukuta mwanamke hana,hili huwezi kulijua hadi pale utakapokuwa na umri fulani kwasababu utakuwa umeshakutana na vituko hivi mara kwa mara na utakuwa umejifunza
Kuna wengine hata mwanamke akiwa na ujauzito halafu akawa hali vyakula fulani basi kwao linakuwa ni tatizo kwasababu hawajui kama unauzito unasababisha haya na akijifungua yote yanakwisha,suala hili linataka kufanana na hili lako...
Wanawake kununa na kususa ni kama kawaida yao na hili unapaswa kulijua,mnapotofautiana na mkeo/mpenzi wako na akanuna wewe usijali wala usionekane kukwazika bali wewe chukulia kawaida tu na atarudi mwenyewe kwenye hali ya kawaida na kama ni kubadilika atabadilika mwenyewe bila shuruti kabisa
Wakati mwingine anafanya hivyo ili kutafuta attention kutoka kwako baasi,sasa wewe ukihamanika utaharibu mambo zaidi,ndio maana wakati mwingine kuwa na mke kwenye umri huo mdogo ni hasara sana kwasababu unakuwa hujui baadhi ya mambo ya msingi!!