Habari wana jf, hii mara yangu ya kwanza kupost kuomba ushauri na ninaomba ushirikiano.
Miezi miwili iliyopita nimekuwa na uhusiano na mwanaume ambaye anaonekana kunipenda na mimi ninampenda sanaaa.Tatizo ni kuwa mpenzi wangu nilimpata nikiwa na mahusiano na mtu mwingine ambaye nilimwacha baada ya kuona sina mapenzi nae ya kweli, huyu mpnz wangu nae alikuwa na mahusiano na mwingine,lakini hakuwahi kuachana nae japo hawakuwa na mawasiliano mazuri,zaidi ya yote ananiambia hana mpango nae ila msichana huwa anamtafuta mwanaume na kumtaka wakutane ila mwanaume anakataa ila hawezi kumwambia waachane,hofu yangu ni kuwa siku moja watarudiana maana hawajaachana. Siwezi kumwambia kwa lazima amuache ila naona anamuonea huruma kumwacha. Naombeni ushauri maana ninampenda na sitamani hata kumkosa yani, nahofia siku wakikutana watapendana upya.
Picha moja stelingi wawili umeona wapi? Kama anakupenda kweli hakikisha amepiga chini huo mpango mwingine.
hapo sasa ni wewe kuwa na makeke kama kweli unahitaji kuwa na future nae... awezi fanya maamuzi ya kumwacha mpenzi wake kama ataona na wewe ni mzigo jitume deka mjali mpende akisha kaa kwenye mstari tulia sasa acha kazi kwake
Una hakika hawakutani?
Hapo amekuwezea kweli kweli.... Ni namna tu ya kukufanya usijisikie vibay zaidi ukijakuwagundua.. Hapo wanaendelea kama kawaida.
Kati yako na yeye nani alimuanza mwenzie? ( kuanzisha mahusiano).sina uhakika ila ninamuamini tuu kwa asemayo
Wengine unapompenda,kudeka na kuwa na makeke ndiyo unazidi kumboa.hapo sasa ni wewe kuwa na makeke kama kweli unahitaji kuwa na future nae... awezi fanya maamuzi ya kumwacha mpenzi wake kama ataona na wewe ni mzigo jitume deka mjali mpende akisha kaa kwenye mstari tulia sasa acha kazi kwake
Wengine unapompenda,kudeka na kuwa na makeke ndiyo unazidi kumboa.