Ananipenda ila aliumizwa sana, naogopa kumuumiza tena

Socw

JF-Expert Member
Aug 27, 2016
1,329
2,644
wakuu!
Nilikutana na msichana katika mazingira flani hivi ambapo kila siku ilikuwa lazima tuonane, na tukazoeana na ikafika wakati nikamwambia kuwa nampenda, hakunizungusha sana akakubali. ki umri yeye amenizidi miaka mitano na akaja akaniambia kuwa amezaa mtoto mmoja ila inaonesha aliachana na mzazi mwenzie kwa ugomvi mkubwa. Na imepelekea kuharibika kisaikolojia na kuwa mwenye kukasirika mara kwa mara na mara nyingi amekuwa akinambia kuwa anatamani siku akawaue baba na mtoto wake ili apoze machungu. Mimi sikumpenda haswa kwa sababu kwanza siyo mzuri kivile pia ana tabia ya kukasirika kwa vitu vidogo japokuwa hasira yake huwa haidumu kwa muda mrefu..ila yeye amekolea na mimi. Nataka kumwacha lakini najiuliza yeye atakuwa katika hali gani...maana tangu aumizwe mimi ndiye mtu wake wa kwanza so ataumia sana...nifanyaje?
 
kuwa mvumilivu kama ulishajua matatizo yake nenda nae taratibu atakaa sawa ,ila ukimwacha utamsababishia matatizo makubwa
 
wakuu!
Nilikutana na msichana katika mazingira flani hivi ambapo kila siku ilikuwa lazima tuonane, na tukazoeana na ikafika wakati nikamwambia kuwa nampenda, hakunizungusha sana akakubali. ki umri yeye amenizidi miaka mitano na akaja akaniambia kuwa amezaa mtoto mmoja ila inaonesha aliachana na mzazi mwenzie kwa ugomvi mkubwa. Na imepelekea kuharibika kisaikolojia na kuwa mwenye kukasirika mara kwa mara na mara nyingi amekuwa akinambia kuwa anatamani siku akawaue baba na mtoto wake ili apoze machungu. Mimi sikumpenda haswa kwa sababu kwanza siyo mzuri kivile pia ana tabia ya kukasirika kwa vitu vidogo japokuwa hasira yake huwa haidumu kwa muda mrefu..ila yeye amekolea na mimi. Nataka kumwacha lakini najiuliza yeye atakuwa katika hali gani...maana tangu aumizwe mimi ndiye mtu wake wa kwanza so ataumia sana...nifanyaje?
Ushaandaa kaburi na will?
Kama kawaza hadi kumuua mwanae we ukimuacha tu shingo yako halali yake..
RIP to be boss
 
she needs psychological advice maana hiyo kutaka kuua mtoto wake ili apoze machungu loohhh!!

mi nasemaga hivi tujifunze kukubali matokeo pindi mkiachana ukihold grudges ndo hvyo at the end of the day unakua mtu wa hasira hasira and people can't stand u at all...!!
 
Hasira humfanya mtu kufikiria mengi zaidi, kaaa nae vizuri mtoleee wazo la kuua kwani sio vizuri.
Harafu unatakiwa umuoe pengine ikawa ndo neema kwako.
 
Ndo kukurupuka kwenyewe huko! Kwanini Ulimtongoza wakati humpendi na unafahamu maumivu yake??? We ni walewale tu. Mwache umuongezee machungu dada wa watu. Kama hutaki kumuumiza mtu acha kukurupuka kwenye kutongoza
 
Faraja nakuita faraja hata ukae nami mwaka mmoja faraja ili faraja ikae kwangu nae faraja awe mfariji wangu. Hivyo naomba usimwache tambua ameadhirika kisaikolojia
 
Wakati unamtongoza si ulimwambia mwenyewe unampenda?iweje sasa leo eti haumpendi?vijana wwngine ni vizazi vya nyoka,umuumize mwenzako kwa maslai yako binafsi,.
 
Yaani huwa nashindwaga kuwaelewa wanaume kabisaa!!!!
Wakati unamtongoza ulimwambiaje labda, usiwe na akili za kivulana, ungemwambia toka mwanzo kabisaa kabla hajakupenda mazima.
Hebu jiweke kwenye nafasi yake sasa hivi uhisi hayo maumivu yake.
Usiwe unacheza na hisia za binadamu wenzako, mwambie sasa ili aumie uridhike maana ndo lilikuwa lengo lako lakini sasa unataka tukuone mtakatifu
 
Angalia hisia zako
Ukiangalia eti huwezi kumuacha kisa atakuwa kwenye hali gani hapo unakuwa unafeli

Mpe ukweli kama akiweza muwe marafiki wa kawaida
 
Back
Top Bottom