Ananiomba Msamaha-ushauri wenu please

Ananiomba Msamaha-ushauri wenu please

B.G TANTAWI

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
496
Reaction score
379
Wadau

Kama mtakumbuka mwaka huu mwanzoni nilileta hapa post ikisema:-Umechelewa Kuleta Posa.

Wataalamu watauweka hapa ili kujikumbuka, Sasa juma mosi ya juzi nilipata ujumbe mfupi wa simu "Mambo"? kucheki naona ni yule yule binti (Mkurya) katuma, bila hiyana nikajibu "poa" akatuma tena "Bado nakupenda sana nisamehe kwa yote niliyokutendea" nikamuuliza yapi hayo uliyonitendea?

Akapiga simu, akasema, naomba unisamehe najua nilikuudhi but naomba tuendelee na mahusiano, nikamuuliza, Umemaliza? akasema yeah, nikasema "Kila la kheri" nikakata simu.


Sasa toka siku hyo anapiga simu sana na kutuma sms but si-respond, kiufupi ni kuwa huyu binti alikuwa mchumba wangu, sasa wakati najiandaa kupeleka posa kwao kwamba kesho yake ndo napeleka, akanipigia cm kuwa wameahirisha kupokea posa yangu kisa eti nimechelewa.

Sasa toka mwezi wa 5 nikaona nitulie kwanza akili yangu ijitulize wakati nikiendelea kutafuta mwingine taratibu, coz baada ya hii sintofahamu nikapanga kuwa nitaoa mwakani na mwaka huu nitafute mchumba mwingine.

Huyu binti moyo unasita sana na sijui wala sidhani kama nitarudiana naye coz kwanza aliniahibisha kwa ndugu zangu, pili:-hivi kwanza hata nikikubali nitaonekanaje kwa wazazi wake maana na wao walishadidia sana kuwa nimechelewa.

Ushauri wenu wadau.
 
Mie nakushauri sikiliza/fata moyo wako unavyotaka, kama unaona huwezi kurudiana nae basi mpotezee tu
 
Kama kweli humtaki Kwanini usimwambie tayari umekwishaoa, tena wake wawili. Inaonyesha wewe ni nataka sitaki. Uwanaume kazi kweli kweli.
 
Ushauri mfupi tuu fuata moyo wako unavyokuambia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom