Nissan Xtrail ni moja kati ya magari imara, huu ni mwaka wa 3 nina Nissan Xtrail, zaidi ya Service za kawaida nilichokibadilisha ni Air Filter na nimeibadilisha baada ya kuiona imekaa sana lakini bado ilikuwa kwenye hali nzuri.
Hata Break Pads baada ya km kadhaa fundi akasema kwenye km kama 8,000 itabidi uzibadilishe, ilipofikia km 8,500 nilihamua kununua Break Pads mpya(genuine) za mbele na za nyuma lakini nilipoipeleka kwa fundi kucheki akakuta bado sana, yaani kama nusu ya pads ndio zimeondoka.
Kwa kufupi Nissan Xtrail ni moja ya magari imara sana