Anachokifanya Rais Magufuli ni Suicide kwa CCM

tajirijasiri

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,863
3,852
CCM imekuwa ikiongozwa kwa mifumo ya mitandao ya watu. Na ni mitandao hiyo hiyo imekuwa ikiwezesha ushindi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge, madiwani na hata ule wa Mitaa.

Kitendo cha Rais Magufuli kuamua kupambana na rushwa na Ufisadi a.k.a kutumbua majipu, kunaua mtandao uliojiotea mizizi ndani ya CCM. Na kwa hakika ni kujiua kwa mikakati ovu ya uchakachuaji wa matokeo ya chaguzi mbali mbali nchini ulioasisiwa na CCM.

Endelea hivyo hivyo Rais Magufuli ili 2020, Uchaguzi Mkuu uwe huru na haki, usioendekeza rushwa na Ufisadi wa wana mtandao wa CCM. Na ushindi halali wa Rais, Wabunge na Madiwani upatikane.

CCM is killing itself a.k.a Suicide a.k.a inajiua yenyewe.

"Upinzani wa Kweli utatoka ndani ya CCM" JK Nyerere. Yametimia.

Sijui naeleweka?

Nawasilisha.
 
Mitandao imekufa rasmi baada ya JPM kuwa rais. CCM inazaliwa upya, kwa maana kwamba fikra za urafiki, kujuana na kuishi kwa makundi, ni mambo ambayo hayawezi kupewa nafasi kwa sasa. Wale ambao walikuwa wafuasi wa yale makundi mawili yaliyotishia kuivunja CCM, hawawezi tena kuwa na nguvu ya kujikusanya na kuufikiria urais. Lowassa yupo upinzani, uwezekano wa Membe kuutafuta urais mwaka 2025 ni mdogo sana. JK anamalizia muda wake wa uongozi, CCM wapo kwenye nafasi ya kujikusanya na kuishi kinyume na dhambi ya ubaguzi ambayo madhara yake wanayajua vilivyo.
 
Nguvu ya upinzani ilitokana na mfumo huo wa CCM. Kubadilika kwa mfumo ni kifo cha upinzani. Unapofanya uchambuzi tazama na upande wa pili.
 
Nguvu ya upinzani ilitokana na mfumo huo wa CCM. Kubadilika kwa mfumo ni kifo cha upinzani. Unapofanya uchambuzi tazama na upande wa pili.
Upinzani upi unaouongelea, zaidi ya Upinzani wa kweli unaotoka ndani ya CCM yenyewe ambao umeasisiswa na Magufuli mwenyewe dhidi ya Chama Chake mwenyewe?
 
CCM imekuwa ikiongozwa kwa mifumo ya mitandao ya watu. Na ni mitandao hiyo hiyo imekuwa ikiwezesha ushindi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge, madiwani na hata ule wa Mitaa.

Kitendo cha Rais Magufuli kuamua kupambana na rushwa na Ufisadi a.k.a kutumbua majipu, kunaua mtandao uliojiotea mizizi ndani ya CCM. Na kwa hakika ni kujiua kwa mikakati ovu ya uchakachuaji wa matokeo ya chaguzi mbali mbali nchini ulioasisiwa na CCM.

Endelea hivyo hivyo Rais Magufuli ili 2020, Uchaguzi Mkuu uwe huru na haki, usioendekeza rushwa na Ufisadi wa wana mtandao wa CCM. Na ushindi halali wa Rais, Wabunge na Madiwani upatikane.

CCM is killing itself a.k.a Suicide a.k.a inajiua yenyewe.

"Upinzani wa Kweli utatoka ndani ya CCM" JK Nyerere. Yametimia.

Sijui naeleweka?

Nawasilisha.
Isije ikawa unamtisha kiujanja Rais ili apunguze makali?
 
Mitandao imekufa rasmi baada ya JPM kuwa rais. CCM inazaliwa upya, kwa maana kwamba fikra za urafiki, kujuana na kuishi kwa makundi, ni mambo ambayo hayawezi kupewa nafasi kwa sasa. Wale ambao walikuwa wafuasi wa yale makundi mawili yaliyotishia kuivunja CCM, hawawezi tena kuwa na nguvu ya kujikusanya na kuufikiria urais. Lowassa yupo upinzani, uwezekano wa Membe kuutafuta urais mwaka 2025 ni mdogo sana. JK anamalizia muda wake wa uongozi, CCM wapo kwenye nafasi ya kujikusanya na kuishi kinyume na dhambi ya ubaguzi ambayo madhara yake wanayajua vilivyo.
Nchi ambayo watu wake wengi hawajasoma hawaangalii performance mkuu bali una nini kipindi cha kampeni.CCM kipindi cha kampeni wanachangisha wafanyabiashara kuanzia laki huku mitaani ndiyo maana kila nyumba wanatoa kuanzia buku mbili ila 2020 Wafanyabiashara wameshagawanywa na vyama vya upinzani hivyo watakuwa taabani kiuchumi
 
Nguvu ya upinzani ilitokana na mfumo huo wa CCM. Kubadilika kwa mfumo ni kifo cha upinzani. Unapofanya uchambuzi tazama na upande wa pili.
Mwambie abane zaidi mianya ya upigaji alafu subiri 2020 utakiona maana ya siasa
 
HAKUNA KITAKACHOSHINDANA NA CHAGUO LA MUNGU

CHADOMO 2015 WALINUNULIWA WOTE KUANZIA DJ MPAKA NYUMBU

LAKINI CHAGUO LA MUNGU NA UMMA WA WATANZANIA LILIKUWA NI MAGUFULI

HATA 2020 ITAKUWA VIVYO HIVYO
 
Upinzani hauwezi kufa ila strategies zinabadilika mpaka sasa magufuli anasafisha bado hajaanza kupanga ya kwake mwenyewe tusubiri tuone
 
Mpwa umeeleweka ila nadhani huwajui CCM walivyo, inapokuja suala la maslahi yao sio ya nchi nazungumzia maslahi yao, huwawezi kabisa, wanaungana na kuwa kitu kimoja kisha wakishapata wanalotaka wanatawanyika tena, kuna yule kiumbe mwenye uwezo wa kujpanda mwenyewe! Yaani yeye ana jinsia ya KE na ME kwahio ndio hivyo walivyo, baada ya tendo kila mtu hurudia status yake. au yule mdudu/mnyama (konokono?) ambaye akayemuwahi kumpanda mwenzie ndio atageuka kuwa jike na kulea mayai na watoto..... chunguza sana utaelewa ninachomaanisha. linapokuja suala la reproduction kwa CCM hawaangalii hiki wala kile, atakyewahiwa ndio atatiwa mimba!
 
Nguvu ya upinzani ilitokana na mfumo huo wa CCM. Kubadilika kwa mfumo ni kifo cha upinzani. Unapofanya uchambuzi tazama na upande wa pili.

Upinzani haufi kamwe bali utaimarika zaidi kwa kutoa mawazo mbadala ya mifumo na kisera badala ya hali ilivyo sasa ambapo dira yote imeeelekezwa kwa unyang'au na ufisadi. Mifumo ya kutatua changamoto inayomzunguka binadamu ni mingi, hivyo kukubaliana na mfumo moja haitatokea (isipokuwa kama nchi inaendeshwa kwa udikteta).
 
Kilichokuwa kinafanya CCM wachakachue chaguzi ni kwa sababu ya huo ufisadi ambao watu waliuchoka. Upinzani ukachukua agenda ya ufisadi kuwa ndiyo kete yake. Kwa Magufuli kuondoa kero hiyo, 2020 hawatahitaji kuchakachua kwani sababu ya watu kuwachukia itaondoka.

Upinzania wanatakiwa kuwa smart watafute agenda nyingine la sivyo watakosa cha kuwauzia wananchi.
 
Watu walioupotosha upande wa UKAWA kuamini watashinda na Edo na baada ya kushindwa kwa mbali wanadhani baada ya miaka mi5 wataibuka tena imekula kwao!
Asilimia kubwa wamejigeuza wapiga ramli na watabiri fake maskini! Kutabiri mwisho wa utendaji wa Mh. Magufuli au CCM atakayoiongoza ni kuamua kuwa shoga wakati unaishi na wanawake watupu. Hutapata wafuasi!
Msijidharirishe bure jamani! Mh. Magufuli ni namba nyingine!
 
Back
Top Bottom