TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
Hakuna aliyepinga Zitto Kabwe kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa. Dharau aliyoionesha waziwazi kwa viongozi wa Chama chake hicho cha zamani na kwa mwenyekiti wake, taifa ndizo hazikukubalika hata kidogo kwa watiifu wote wa Chama.
CHADEMA kwa sababu ya uchanga wa Demokrasia na udogo wa Chama chenyewe , hawakuwa na kifua cha uvumilivu, waliamua kumtimua yeye na wote waliokuwa nyuma yake. Watu wengi tulipiga kelele kupinga hatua zilizochukuliwa dhidi ya Zitto.
Anachokifanya Nape Moses Nnauye kwa chama chake cha Mapinduzi na kwa mwenyekiti wake wa taifa hakina tofauti na alochokuwa anakifanya Zitto Kabwe. Tofauti na CHADEMA, CCM ni chama kikongwe, kikomavu kisiasa, chenye demokrasia ya hali ya juu na Chama kikubwa. Hakuna namna yoyote ya kumfanya Nnape Nnauye bali kumuacha afuate nyayo za akina Edward Lowassa , Hamisi Mngeja na watu wengine wa kariba hiyo.
Ni wazi NAPE alifikiri kwa alipofikia Mwenyekiti wa CCM siyo chochote wala lolote kwake. Pengine alikuwa na ndoto za kuwa Mwenyekiti maana kama Mwenyekiti wako humuheshimu basi lazima utajiona wewe ndiye.
Ushauri wangu kwa Nape: Muda ndiyo huu, aondoke akiache chama na wote wanaomtii mwenyekiti wa CCM, taifa.
Ni hayo tu kwa leo