Fahari ya kusini
JF-Expert Member
- Nov 26, 2022
- 427
- 1,668
Ameandika Bobi Wine, Mwenyekiti wa Chama cha NUP na Mbunge wa zamani wa jimbo la Kyadondo.
_________
Kwa huzuni kuu na mioyo mizito tunasikitika kutangaza kifo cha cha mpendwa wetu, mwanaharakati na rafiki, Marinos Alexandros. Marinos alitekwa nyara tar 30 Machi 2022 akiwa nyumbani kwake Mbuya, jijini Kampala. Alipelekwa kambi ya mateso kwenye kituo cha kijeshi cha CMI Mbuya, ambapo alipigwa na kupewa mateso makali ikiwemo kuwekewa shoti ya umeme. Wahuni hao hawakuishia hapo walimbaka pia 😭.
Kosa lake ni kuwa mwanachama wa NUP na kumuunga mkono Bobi Wine. Alituhumiwa pia kumkosoa Rais Museveni hadharani (watekaji wanasema alimtukana Rais, maana hawajui tofauti ya kukosoa na kutukana). Pia kosa jingine ni kukaidi amri aliyopewa ya kumzuia kupiga muziki wa Bobi Wine kwa spika za sauti.
Baada ya mateso makali walimtupa katika ufukwe wa Port Bell akiwa amepoteza fahamu. Aliokotwa kesho yake na kukimbizwa hospitali kwa matibabu na ikabainika alidungwa sindano ya sumu pia. Alipotoka alifanya press kufichua wahalifu hao. Baada ya hapo alianza kupokea simu za vitisho vya kuuawa. Nyumba yake ilivamiwa usiku na watekaji, ambao walivunja mlango na kuingia ndani, lakini kwa bahati nzuri hakuwepo. Alikuwa amelala kwa rafiki yake.
Hali hiyo ilimlazimu kukimbia nchi yake na kutafuta hifadhi Nairobi – Kenya. Lakini hata akiwa Kenya, wahuni walijaribu kumteka tena, hali iliyomfanya aondoke Nairobi na kuelekea kwenye kambi ya UNHCR ambako angepata usalama zaidi. Hali yake kiafya ilizidi kuzorota na alipopimwa ndipo ikabainika kuwa wahuni wale walipombaka walimwambukiza pia virusi vya UKIMWI.
Mwaka jana afya yake ilidhoofika sana na akaanza kupatiwa matibabu huku tukimsaidia. Kwa sababu ya upweke na hali ngumu katika kambi ya wakimbizi, aliamua kurejea Uganda wiki chache zilizopita ili kupata matibabu bora akiwa karibu na familia yake.
Ni jambo la kusikitisha sana kwamba tumempoteza leo saa 1:30 asubuhi akiendelea na matibabu. Marinos amejiunga na mamia ya wahanga wengine wa utawala wa damu na hofu wa Rais Museveni.
Kwaheri kamanda. Mapambano ya uhuru na demokrasia nchini Uganda yamepoteza nguzo muhimu, lakini utawala wa kishetani wa Museveni hautapata kicheko cha mwisho.!