Sijui sana kuhusu Ole Sendeka, ila Anna Kilango ni rafiki wa karibu sana na spika Anne Makinda. Kwenye arusi yake na Mzee Malecela, Anne Makinda ndiye aliyekuwa matron wake. Sasa hapo si unaonatunavyopigwa changa la moto? Kuna katabaka ka watu walioko kwenye madaraka ambao hata hizo kelele za kujivua magamba inakuwa kama kelele za chura kwenye maji. Kwa kifupi ni usanii wa ccm, nia na madhumuni yao ni kuigeuza nchi yetu kuwa ya kisultani. Vyeo vitaendelea kutolewa kwa majina. Anna Kilango amekumbuka kuwa yeye ni Mama Malecela, na ni swahiba wa spika! Kaaaaaazi kweli kweli!