Amuua mwenzake kwa kipigo baada ya kumkuta akimtongoza dada yake

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Mkazi wa kijiji cha Kalovya – Inyonga wilayani Mlele, Ramadhani Ally (20) amefariki dunia akipatiwa matibabu hospitalini baada kupigwa na kijana mwenzake.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahri Kidavashari amesema kuwa Ramadhani alifikwa na umauti baada ya kujeruhiwa na kijana mwenzake Ntema Kabembenya( 26), mkazi wa kijiji cha Ipwaga.

Kidavashari amesema tukio hilo lilitokea Januari 22, mwaka huu saa 12:55 jioni ambapo Ntema alimkuta Ramadhani (marehemu) akimtongoza dada yake (Ntemwa) mwenye umri wa miaka 12 (jina limehifadhiwa).

“Ntemwa alikasirishwa na kitendo cha Ramadhani kumtongoza dada yake mwenye umri wa miaka 12, alimshambulia Ramadhani kwa kumpiga na fimbo na kumjeruhi vibaya,” alieleza Kamanda Kidavashari.

Inadaiwa Ramadhani alikimbizwa katika Hospitali ya wilaya ya Mlele kwa matibabu lakini alifariki dunia siku iliyofuata akiwa anatibiwa.

Kwa mujibu wa Kidavashari, mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi ambapo anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.
 
Hana kesi ya kujibu, Marehemu alikuwa anaelekea kubaka mtoto (12 yrs)
Hakubaka. Alikuwa anaelekea. Je, anatakiwa kuuawa? Nani anaweza kuthibitisha alikuwa anatongoza? Ni hilo tu ndio lilimsababishia kuua. Halafu unasema HANA KESI YA KUJIBU. Yaani rahisi hivyo!
 
Safi sana Ntema, Jogoo wenyewe hawapandi vifaranga!! marehemu kazidiwa akili mpaka na kuku.safi sana tangulia...
 
Ingekuwa Wale Wenzentu Wenye Uwezo Kifedha, Hapo Hakuna Kesi!! ILA Kwa Makabwela Ni SHIDA Kubwa!!!
 
Siku zote unatakiwa kujitahidi kuzuia hasira katika jambo lolote lenye kukuudhi kwani bila kufanya hivyo unaweza kujikuta maneno, ndoto zako zote zinavurugika baada ya kuwa umeingia kwenye matatizo mkubwa yaliyosababishwa na wewe mwenyewe kushindwa kuzuia hasira zako
 
Kwa sheria za nchi gani hana kesi ya kujibu?
Mkuu Chachu!
Asante sana kwa nyuzi kwa wale wasiojua kitu wanatawaliwa na Giza katika macho yako.
Ulivyomuuliza yule anaesema mshitakiwa hana kesi nitatilia mkazo hoja kwa kumuuliza kuna sheria yoyote inayomruhusu mtu kumuadhibu mtu mwingine amkutapo akitenda kosa?
Endelea kusoma maoni ya Bush lawyers ushangae na uelewa wao duni wa Sheria.
 
Back
Top Bottom