diana chumbikino
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 428
- 368
MKAZI wa Kijiji cha Idete-B, Anna Msangi (26) wilayani Kilombero, mkoani Morogoro anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuua kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali kwenye titi Katarina Mangomile (30) aliyemtuhumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mumewe.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Wilbroad Mutafungwa alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Jaunari 2, saa sita usiku katika kijiji hicho ambapo mtuhumiwa alimchoma kifuani chini ya titi la kushoto Katarina. Kamanda Mutafungwa alisema baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali alikimbizwa hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Francis Ifakara na aligundulika alikuwa ameshafariki. “Chanzo cha tukio hilo Kamanda,” alisema, “ni wivu wa mapenzi ambapo marehemu enzi za uhai wake alikuwa akilalamikiwa na mtuhumiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mumewe Anna.
“Alipomuona Katarina yuko na mumewe alihisi wana mauhusiano na ndipo alimchoma na kitu chenye ncha kali na kusababisha mauti yake,”alisema Kamanda Mutafungwa. Hata hivyo, Kamanda Mutafungwa alisema mtuhumiwa anahojiwa kuhusiana na kosa hilo na mara upelekezi utakapokamilika atakishwa mahakamkani. Katika hatu nyingine, Kamanda Mutafungwa alitoa mwito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwani hivi karibuni kumeibuka wimbi la mauaji yanayosababishwa na wivu wa mapenzi.
Mauaji hayo ni ya pili kutokea ndani ya siku 10, mkoani hamu ambapo tukio la kwanza lilitokea alfajiri ya kuamkia Disemba 25, mwaka jana katika kijiji cha Mkula, Wilaya ya Kilombero, mkazi wa Dar es Salaam aliyefahamika kwa jina maarufu la Msambaa kudaiwa kumuua kwa kumchoma na kisu sehemu mbalimbali za mwili wake mzazi mwezie, Zuhura Chunga (27), mkazi wa kijiji hicho kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa mapenzi na baada ya kutekeleza unyama huo mtuhumiwa alitoroka.