Amuua mumewe kwa sumu ili afunge adoa na mchepuko

Amuua mumewe kwa sumu ili afunge adoa na mchepuko

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,741
Reaction score
25,681
image-78_4.png
MWANAMKE mfanyakazi katika gereza kutoka Missouri, Marekani anatuhumiwa kuwa alimuua mumewe kwa kumtilia sumu kwenye chakula, ili waoane na mpenzi wake mfungwa. Amy Murray, wa miaka 40 alishtakiwa Ijumaa kwa mauaji ya mumewe Joshua Murray wa miaka 37, ambaye alipatikana akiwa maiti mnamo Desemba 11.





Japo mwanamume huyo alipatikana kitandani akiwa maiti, ripoti ya upasuaji wa mwili wake ilionyesha kuwa alikufa kutokana na kutiliwa sumu, kabla ya mtoto kuwashwa ndani ya nyumba yake. Ni hapo ambapo wachunguzi katika kesi hiyo walibaini kuwa Amy alikuwa akifanya kazi ya uuguzi katika jela ya Jefferson na alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mfungwa Eugene Claypool, wa miaka 40.


amy-murray.jpg



Amy anasemekana kuanzisha moto huo kisha akaondoka nyumbani kwake na mwanawe mvulana na mbwa wawili. Lakini mshukiwa alieleza wachunguzi kuwa aliporejea nyumbani alipata nyumba ikiwaka moto na moshi ulikuwa mkubwa hivi kwamba hangeweza kuingia.





Lakini wachunguzi walipata rekodi ya mawasiliano baina ya Amy na mpenzi wake mfungwa, ambapo alikuwa akimwambia kuwa hakutaka tena kuwa katika uhusiano wa ndoa na mumewe. Katika mawasiliano mengine, alimwambia Claypool kuwa angemuoa kwa kuwa mumewe sasa alikuwa amefariki na hangezuia kitu.





Wawili hao aidha walizungumzia kuhusu kumtafutia mfungwa huyo wakili ili aachiliwe mapema. Claypool alikamatwa mnamo 2000 na amekuwa gerezani kwa zaidi ya miaka 18, kwa kosa la kumdunga kisu mwanamume wa miaka 72 ambaye alishinda zaidi ya Sh100milioni katika mchezo wa Kamari. Amy na mumewe Joshua walikuwa wameoana tangu 2003 na walikuwa na mtoto wa kiume.
 
Too sad[emoji26]
Hakika asipotubu dhambi itamtafuna
Hata Kama atatubu bado madhara ya dhambi yake Ni makubwa
Mungu husamehe dhambi Ila madhara ya dhambi yanaweza yasisamehewe
(Jela)

Kwanini asiachane nae tu!??aisee wanawake wengine Kama mashetani
Kwenda kuangamiza damu isiyokuwa na hatia..kumdhulumu mtu pumzi[emoji26]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanawake wanawake wanawake jamani wanawake hawa wananwake ndo maana Mungu alimuita mwana mke Hawa yaan hawa wanawake hawa dah
 
Askari Magereza - Muuguzi anatumia Wodi za wagonjwa Gerezani kama G.House na kufanya yao hadi kunogewa na kupanga kuoana kwa kumuua mume.

Kwa Wajomba haya wanapotezea, wanaona kuwa ni kosa la mtu, je ingekuwa ni TZ

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom