Habari zenu wana jamvini ninarafiki yangu alikua na mchumba wake na alikua amesha mtolea mahari tena mahali ndefu iligharimu 2000000 kipindi wanaanza mahusiano Dada wa watu alionesha tabia nzuri upole, unyekevu, heshima, upendo kwa watu wakaribu wa jamaa yetu pamoja na kujiheshimu kiukweli alionekana wife material ikafika kipindi tukamtia moyo jamaa yetu kumuoa yule binti kwani hakuonekana na matatizo. Baada ya kumtolea mahari akaanza kuonyesha matatizo siku moja ndipo alipo mkuta yuko na rafiki zake wa kike watatu na jamaa watatu wanakunywa bia huku yeye akiwa amesima anakata viuno ameva suruali zile za condom na kibrauzi kilichoacha mgongo na tumbo nje. Toka enzi za uchumba wao alikua akivaa nguo za stara. Jamaa kaamua kuachana nae ingawa dem anaomba asamehewe na wazazi wa binti wanamsi jamaa amsamehe binti yao je kwamaoni yako alicho kifanya jamaa yangu ni cha busara au amekurupuka nawakirisha