Dada yetu anaishi na Virusi vya UKIMWI, tumwambie ukweli mchumba wake?

navin-govind

Member
Apr 10, 2015
72
112
Habari zenu wana Jf,

Nina mdogo wangu wa kike baba mmoja ila mama ndio tofauti, mzee alikua na wake wawili. Huyu binti alikuwa akifanya biashara za kusafiri kwenda Kampala na Nairobi kwa miaka mingi, ni mdogo wangu wa nne kuzaliwa, tupo tisa kwa hao mama wawili, ila mama zetu hawapo duniani, mzee ndio bado yupo katika hizi safari za kibiashara bahati mbaya akapata ugonjwa huu wa kisasa, aliugua sana hapo katikati, nadhani ilikua 2006-2009.

Baadae akapona akainuka kabisa kutoka kitandani lakini akaambiwa asiache dawa za kurefusha maisha, tukamzuia kuendelea na hizo business za kusafiri, akaokoka na bado anaabudu hadi sasa, amenona hasa, amekuwa kipande cha mtu. Simzungumzi vibaya Dada yangu, ila kwa kweli amekuwa na wowowo lenye kumvutia mwanaume yeyote yule.

Nadhani ni katika muonekano huo ndipo akajitokeza mlokole mwenzie huko kanisani kwao kutaka kumuoa, huyo jamaa kachanganyikiwa na yuko resi mno, ameshaniletea barua nami nikaipokea pamoja na wenzangu, baadae tukamtajia mshenga wake mahari nayo akalipa na tulishaila, tuligawana makaka, nae binti tukampa kidogo.

Sisi hatujaanza utaratibu wa vikao ila wao upande wa jamaa walikaa vikao viwili tayari, wakati wote huu mimi nilidhani dada alishamweleza status yake huyu mchumba, na pengine nikadhani wote wana status hiyo hiyo ya HIV positive wameamua ku team up kuunda familia, kumbe sivyo huyu jamaa hajui chochote kuhusu hali ya huyu dada yangu.

Kuna dada yetu mkubwa aliyempeleka kanisani huyu binti na wanasali pamoja, juzi alimuuliza muolewaji kama amemwambia mchumba hali yake, akajibu hajamwambia, anaogopa akimwambia atakosa ndoa, na yeye anahitaji kuwa na familia yake kama mwanamke, na kwamba yeye mwenyewe aachiwe jambo hilo atalimaliza mwenyewe, na kwamba tusimwambie mchumba chochote.

Roho yangu inanisuta sana kushiriki jambo hili, hasa ukichukulia kuwa nyumba na mji wangu ndio unaochukuliwa kama nyumbani kwao na bibi harusi, na tupo karibu sana kimawasiliano na huyo jamaa. Mfano ni juzi tu kanitumia laki mbili akisema ni ya chai.

Pia ni msomi mwenye carrier yake na future inayoeleweka, hivyo nafsi inanisuta, wenzangu wanadai afya za maharusi sio kazi yetu, kwamba sie kazi yetu ni kusherekea tu, kwamba ni miaka sasa hatujawa na harusi tunachangia watu tu.

Wadau, nahitaji msaada wa mawazo

Au na mimi nipotezee tu watajuana wenyewe?
 
Mshauri dada' ko amwambie, kama ananpenda Mungu asikubali kuua damu ISO na hatia kwake. Ndoa c lazima ila kama mchumba wake atakubaliana nae sawa.
 
Usishiriki kwenye hiyo murder case, lazima mhusika aambiwe hiyo issue au jifanye kuwa lazima vipimo vipatikane ndo muibariki hiyo ndoa. Hapo dadaaa hatakuwa na ujanja. Lakini sishauri nyote mkae kimya imagine wewe ndo unafanyiwa hiyo kitu

Ikija chai nyengine ikatae maana mnazidi kumpa matumaini kijana wa watu.
 
Unaweza ukafikisha ujumbe hata kwa njia ya yeyote tu

sio lazima face to face

Unaweza kutuma hata sms kupitia namba ambayo utamtumia au kuongea nae kisha ukaitupa hiyo laini

Mitandao imesaidia sana hapo utabaki unkwown forever

Siri ni ya mtu mmoja tu
 
Hivi ule utaratibu wa walokole kupelekwa na mzee wa kanisa kupima afya na mimba kabla ya ndoa haupo kwenye makanisa mengine? Mimi nakumbuka mke wangu (wakati huo mchumba) alipmwa ujauzito mbele ya mjumbe aliyeteuliwa na kanisa..na baadaye mimi na yeye tulipelekwa hospitali na mjumbe wa kanisa kupimwa maambukizi ya HIV.

Kama kanisani kwao hawana huo utaratibu, na kama kweli hajamfahamisha itakuwa busara kama ukihakikisha jamaa amepata taarifa. Ingekuwa vema kama dada yako angesema mwenyewe, ila yaelekea ameipania ndoa hasa wala hawezi kusema. Hata hivyo sioni kama kutakuwa na ndoa yenye afya baada ya jamaa kugundua kuwa ameoa mwathirika ambaye kwa makusudi kabisa ameamua kuwa kimya na kumwambukiza ugonjwa huo. Kuna hatari ndoa ikavunjika mapema sana na jamaa kuchanganyikiwa au hata kujidhuru.

Yawezekana dada yako anataka tu hadhi ya kuwa na ndoa, kwa maana kwamba hata ikivunjika baada ya siku 2 angalau na yeye atakuwa ameimbiwa "anameremeta", otherwise, sioni ndoa ya kudumu katika mazingira yenye usiri wenye nia ovu kama hiyo.

Kama unaogopa kumwambia shemejio moja kwa moja, tengeneza mazingira ya kijasusi uhakikishe anapata "anonymous message" kumtahadharisha na kusisitiza amwombe mwenzie wakapimwe afya zao kwa ujumla. Kwa vyovyote vile, reaction itakayofuatia baada ya pendekezo hilo itatosha ku-solve kesi hiyo.
 
Habari zenu wana Jf

Nina mdogo wangu Wa kike baba mmoja ila mama ndio tofauti, Mzee alikua na wake wawili
Huyu binti alikua akifanya biashara za kusafiri kwenda Kampala na nairobi kwa miaka mingi, ni mdogo wangu Wa nne kuzaliwa, tupo Tisa kwa hao mama wawili, ila mama zetu hawapo duniani, mzee ndio bado yupo

Katika hizi safari za kibiashara bahati mbaya akapata ugonjwa huu Wa kisasa, aliugua sana hapo katikati, nadhan ilikua 2006-2009 baadae akapona akainuka kabisa kutoka kitandani lakini akaambiwa asiache dawa za kurefusha maisha, tukamzuia kuendelea na hizo business za kusafiri, akaokoka na bado anaabudu hadi sasa, amenona hasa, amekua kipande cha MTU
Simzungumzi vibaya Dada yangu, ila kwa kweli amekua na wowowo lenye kumvutia mwanaume yeyote yule

Nadhan ni katika muonekano huo ndipo akajitokeza mlokole mwenzie huko kanisani kwao kutaka kumuoa, huyo jamaa kachanganyikiwa na yuko resi mno, ameshaniletea barua nami nikaipokea pamoja na wenzangu, baadae tukamtajia mshenga wake mahari nayo akalipa na tulishaila, tuligawana makaka, nae binti tukampa kidogo

Sisi hatujaanza utaratibu Wa vikao ila wao upande Wa jamaa walikaa vikao viwili tayari
Wakati wote huu Mimi nilidhani Dada alishamweleza status yake huyu mchumba, na pengine nikadhani wote wana status hiyo hiyo ya HIV positive wameamua Ku team up kuunda familia, kumbe sivyo huyu jamaa hajui chochote kuhusu hali ya huyu Dada yangu,

Kuna Dada yetu mkubwa aliempeleka kanisani huyu binti na wanasali pamoja, juzi alimuuliza muolewaji kama amemwambia mchumba hali yake, akajibu hajamwambia, anaogopa akimwambia atakosa ndoa, na yy anahitaji kuwa na familia yake kama mwanamke, na kwamba yeye mwenyewe haachiwe jambo hilo atalimaliza mwenyewe, na kwamba tusimwambie mchumba chochote

Roho yangu inanisuta sana kushiriki jambo hili, hasa ukichukulia kuwa nyumba na mji wangu ndio unaochukuliwa kama nyumbani kwao na bibi harusi, na tupo karibu sana kimawasiliano na huyo jamaa
Mfano ni juzi tu kanitumia laki mbili akisema ni ya chai

Pia ni msomi mwenye carrier yake na future inayoeleweka, hivyo nafsi inanisuta
Wenzangu wanadai afya za maharusi sio kazi yetu, kwamba sie kazi yetu ni kusherekea tu, kwamba ni miaka sasa hatujawa na harusi tunachangia watu tu

Wadau, nahitaji msaada Wa mawazo

Au na Mimi nipotezee tu watajuana wenyewe?

Mkuu hapo hakuna problem.
Kaa kimya.
Kwa Kifupi CANCER na KISUKARI ndio hatari zaidi....pia hauambukizi.
 
hata ukimwambia itakua ni kazi bure maana jamaa atakua keshamvua chupi huyo mgonjwa siku nyingi sana.
 
Mmmh, HIV ni ugonjwa hatari, huwezi kukaa kimya kama vile hujui kinachoendelea, japo kweli afya ni jukumu lao wawili. Lakini kama ilivyo kawaida ya makanisa mengi, ni lazima watapewa barua ya kwenda kituo cha afya ili kupimwa HIV( at least kwangu ilikuwa hivyo), then wakirudisha majibu ndipo ndoa itaandikishwa na kutangazwa.
 
Jiulize ingekuwa ww Je inakutokea ishu km hiiii je jaribu Kuwa mkweli usije kushiriki dhambi daaaah inaumaaaaa sanaaaaaaaaa ukweli ndo Kila kitu
 
nafahamu kesi inayofanana na hii. binti alizaliwa na vvu ila hakuwahi kuambiwa japo kuna kipindi aliugua sana. alipoleta mchumba baba mtu akaona si busara kumkatalia binti yake moja kwa moja. siku ya siku akaita kijana na ndugu zake na binti na ndugu zake akawaambia wakapime kwanza ndo mambo ya mahari na taratibu zingine ziendelee. ikabidi watarajiwa wafuate amri ya wajumbe ndo binti akajua status yake.

Huyo dada kwa kuwa anatumia arv uwezekano wa kumwambukiza huyo kaka kama tayari weshazini ni mdogo. Cha kufanya muulize huyo shemeji yako kama walishapima vvu na akikwambia bado msisitize wakapime, akigoma mpasulie ukweli hata kama utaishia kukatwa kichwa kama yohana. mwambie ndo umejua sasa kuwa dadake hajakwambia. hivi siku ya send off au arusi wakati upande wa bwana arusi wanashangilia nyie mtakuwa mnajiskiaje? fanya kitu sahihi. hayo mambo ya vikao na sherehe ni ya kupita kaka.
 
Ndio maana huwa siku zote Nasema kuwa huu ulokole ni.kichaka cha mengi sana! Wewe una ngoma, mtu kakuamini kwa misingi yako unayodai ni ya kiimani, halafu unamficha status yako na kumchagulia maambukizi bila kumshirikisha, hivi hiyo ni akili kweli? Mvute pembeni huyo jamaa, umuulize kama na yeye ana status kama ya dada yako, nikimaanisha kuwa ujifanye ulidhania hivyo. Akijibu tu, mpasulie yote black and white umuachie maamuzi yeye. Im sorry to say this ila sister wako ana roho ngumu sana au amechanganyikiwa kwa kiasi fulani sababu ya upweke. Huwezi kuzungukwa na watu wengi wanaojua status yako na fact kwamba unataka kumwambukiza mtu halafu ujione sawa tu. Mpasulie huyo jamaa, utakuwa unamsaidia na sister wako pia maana ni dhahiri hathink straight!
 
Back
Top Bottom