Amri ya UVCCM

Avocado

Member
Aug 23, 2010
97
4
Hii amri ya kutaka mitambo ya umeme yote iwashwe mara moja,inatolewa na UVSISIEM kwa nani ? Na huo mkwala wanaoutoa kwa mawaziri wakuu wastaafu kuaacha kuikosoa serikali wametumwa na nani ? Hii nchi kweli haina uongozi,viongozi wa juu wa chama chao nadhani wamekufa kwa hiyo vijana wameshika chama na serikali sasa wanatoa AMRI tu ! Kazi ipo !!!
 
Hivi hawa UVCCM wanazungumza kwa niaba ya nani? Hawajui kwamba vijana hapa nchini wamekwisha tambua janja yao yakujineemesha kupitia mgongoni kwao! Ndio maana hivi majuzi walipotaka kupotosha ajenda ya wanafunzi wa vyuo vikuu, wanafunzi hao waliwashutuka na kuwapiga stop. Ni vema wakasoma alama za nyakati, siasa za ubabaishaji zimefikia ukingoni.
 
Back
Top Bottom