Amri kumi za maisha ya ndoa

belionea

JF-Expert Member
Mar 17, 2014
1,046
902


1. Usijitengenezee Mahusiano mengine yanayozidi Mahusiano yako na Mwenzi wako: Pasitokee MTU mwingine (wa jinsia yeyote) ambaye atakuwa na umuhimu wa juu zaidi kuliko mwenzi wako.

2. Usimlinganishe au kumshindanisha Mwenzi wako na mtu mwingine: Kumbuka kila mtu yupo tofauti. Tumia hekima kumsaidia mwenzi wako kuwa bora zaidi pasipo kumfanya ajisikie kwamba hafai au hana viwango unavyotaka wewe.

3. Usitumie Tendo la Ndoa kama fimbo ya kumwadhibu mwenzi wako: Hata kama mmepishana misimamo, kumbuka “Tendo la Ndoa” ni haki ya msingi ya kila mwanandoa.

4. Usiishi maisha ya siri kwa mwenzi wako: Fanya jitihada za makusudi kuvunja kila tabia ya usiri ambayo itasababisha kila mmoja aishi maisha yake binafsi.

5. Usijilaumu kuingia kwenye ndoa au kumuonesha mwenza wako kwamba unaweza pata mbadala wake wakati wowote: Hata kama unahisi “ulichemsha”, sasa fanya wajibu wako kuiboresha hiyo ndoa. Kumbuka UPENDO una nguvu kuliko MAUTI.

6. Usiruhusu kazi au majukumu yako yaidhoofishe ndoa yako: Pamoja na majukumu mengi uliyonayo, hakikisha umuhimu wa ndoa yako unabaki palepale.

7. Usiwe mbinafsi: Usipendelee mambo yako tu au ndugu zako tu; bali kumbuka pia mwenzi wako anao upande wake.

8. Usiwe mwepesi kusambaza mambo yenu binafsi kwa kila mtu: Ndoa ni taasisi yenye kanuni na taratibu zake; mojawapo ya kanuni hizo ni “utunzaji wa mambo nyeti” (Confidentiality). Uwe makini unamwambia nani, kitu gani, wakati gani, na mazingira yapi.

9. Usijidanhaye kwamba kuna mtu mwingine anakupenda zaidi ya mume/mke wako: Kumbuka kuna watu wataonyesha wanakujali sana kwa sababu sasa upo kwenye ndoa; siku ukitoka hutaamini kama ndio wale

10. Usisahu kiapo cha ndoa ni kiapo cha damu na ni kiapo cha maisha: Usiruhusu mawazo ya kutengana au kuachana yawe RAHISI na MEPESI sana ndani ya kichwa na moyo wako. Mara zote katika changamoto jikumbushe KIAPO CHA NDOA… “Nitakuwa nawe katika hali zote…!!”

NB:
Paleka shida zako kwa MUNGU kabla hujazipeleka kwa MARAFIKI au WAPAMBE.

Msaidie mwenzi wako kwa UPOLE na UVUMILIVU awe jinsi ambavyo ungependa awe.

Usitumie KINYWA au MANENO yako kuilaani NDOA yako… bali tamka BARAKA katika ndoa yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HUSILAZIMISHE NDOA: ndoa ikigoma achana nayo kabisa mambo ya kujipa matumaini kwamba eti 'ntamfundisha' 'ntambadilisha' 'na mpa mda' 'ntawaeleza ndugu zake na wazazi' hayo yote ni kulea tatizo na kupoteza mda mtu mzima habadilishwi.....be strong enough fanya maamuzi ya kujinusua

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom