Amrefu kutumia bilioni 25 kuboresha afya ya jamii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amrefu kutumia bilioni 25 kuboresha afya ya jamii

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sumasuma, Feb 10, 2012.

 1. sumasuma

  sumasuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 331
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Furaha Maugo
  SHIRIKA la Utafiti wa Afya na Tiba Afrika(AMREF), limetangaza kutumia zaidi ya Dola 16 milioni za Marekani sawa na takribani Sh25 bilioni, kwa ajili ya utekelezaji wa mpango mkakati wa kuboresha huduma za afya nchini.

  Mpango huo wa AMREF umekuja wakati Ripoti ya Utafiti iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO), hivi karibuni, ikionyesha katika asilimia 20 ya watu wanaojifungua asilimia 40 ya vifo vya uzazi vinavyotokea huweza kuzuilika ikiwa zitapatikana huduma nzuri ya afya kwa wakati.

  Akizungumza katika uzinduzi wa mpango huo jijini Dar es Salaam, Naibu Meneja Mkazi AMREF, Dk Florence Temu alisema kuwa mpango huo ulianza Oktoba mwaka 2011 kwa kutoa mafunzo ya afya ya uzazi kwa wadau husika na unatarajiwa kukatakamilika mwaka 2014.

  Alifafanua kuwa utekelezaji wa mpango huo umejikita katika maeneo makuu saba, aliyosema kwa kiasi kikubwa yatasaidia kuboresha huduma za afya hasa kwa wanawake na watoto pamoja na kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto.

  “Tutajikita katika masuala yanayohusu afya ya uzazi, mama mjamzito na mtoto kwa kuwapatia elimu watu wote wakiwemo wanaume na vijana, jinsi ya kutumia njia za uzazi wa mpango kwa ajili ya kuboresha afya zao na kujikinga na magonjwa mbalimbali, ” alisema Dk Temu.

  Alitaja maeneo mengine yatakayotiliwa ni kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Malaria,Ukimwi na Kifua Kikuu, kuhimiza usafi wa mazingira utakaosaidia kukabiliana na maradhi.

  Awali, akizindua mpango huo Naibu Waziri wa Afya Dk Lucy Nkya, alisema Tanzania bado inakabiliwa na changamoto katika utekezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia hadi kufikia mwaka 2015 akizitaka taasisi za kitaifa na kimataifa kushirikiana na Serikali kutatua matatizo haya.

  “Utawala bora ndio njia pekee itakayowezesha taasisi za watu binafsi,asasi za kiraia na serikali kukabili changamoto za kimaendeleo katika nchi zinazoendelea na wala sio hadi tusibiri misaada kutoka nchi za nje,”alisema Waziri Nkya.:juggle:
   
 2. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Utawala bora gani anaozungumzia Nkya?
   
Loading...