Amka! Maisha na Mafanikio - ya Kifedha

C.K

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
392
160

Katika maisha ya mwanadamu hapa mbele ya jua.., mafanikio ndiyo kitu kinachotafutwa na watu mmoja mmoja na mataifa pia zaidi ya kitu kingine. Mafanikio jamani..!, kiteknolojia, kiuchumi, kielimu, biashara n.k ndiyo haja ya kila mmoja wetu. Ndipo mwanafalsafa maarufu Mohandas Gandhihttp://www.brainyquote.com/quotes/quotes/m/mohandasga160780.htmlhttp://www.brainyquote.com/quotes/quotes/m/mohandasga160780.html akaamua kusema, “mafanikio hatua kwa hatua ni kanuni ya maisha, na mtu yeyote anayejaribu kwenda kinyume ili kulinda mtazamo wake hujikuta katika mwelekeo potofu”. Naye Aristotle anasema “mwanadamu ni mnyama mtafuta mafanikio. Maisha yake yana maana pale tu ambapo anainuka na kupambana ili kufikia malengo yake”.

Yapo mafanikio aina mbalimbali na katika maeneo mbalimbli/tofauti. Lakini kwa sasa nataka tukumbushane kuhusu mafanikio ya kifedha (financial independency). Ukweli suala la kufanikiwa kifedha ni la lazima kama kweli unataka kuishi vizuri hapa sayarini. Fedha-pesa-njululu-mawe-vijisenti... jamani! Kwa nini ni lazima kuwa nazo?! Eti, wewe unafikiri ni kwa nini inakuwa lazima kuwa nazo???! Nadhani haina haja ya kuelezana ulazima wa kuwa na pesa kwani hata kichaa na au mtoto mdogo anajua ulazima wa kuwa nazo. Kufupisha habari, ninataka usome wewe mwenyewe Sura ya kwanza ya kitabu cha Ujasiriamali cha Robert K. niliyoambatanisha. Hiyo ni moja kati ya sura zake tano. Ni cha Kiswahili na kinapatikana Book shops na kwa wauza vitabu – Ubungo, Mwenge, Kariakoo, Posta... Pia baadhi ya mikoa. Kimeandikwa “MAFANIKIO YA KIFEDHA”. Waliokisoma wanajua mambo yake. Kitakuamsha kama ulikuwa umelala katika suala zima la kutafuta pesa – utajiri.


Wewe soma kwanza halafu utaniambia mwenyewe.


Kila la heri!


“kufanikiwa ni maamuzi.., kwa hiyo ukiamua utafanikiwa na kinyume chake ni sahihi”
 

Attachments

  • SURA I - Mafanikio ya Kifedha - JF.pdf
    268.5 KB · Views: 1,050

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Top Bottom