Baada ya kipigo cha siku 12 na Majeshi ya Israel Iran imeamua sasa kuupa jina la Netanyahu mtaa mmoja huko Tehran.
- Tunachokijua
- Madai
Kupitia mitanao mbalimbali ya kijamii kumekuwa na taarifa inayoeleza kuwa Tehran, Iran kuna mtaa umepewa jina la waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
Taarifa hiyo imeambatana na kkipande cha video kinachoonesha kibao hicho chenye lugha ya kiarabu na kiingereza kikisomeka "Netanyahu st". Taarifa hizo zinaendelea kueleza kuwa jambo hilo limetokea mara baada ya vita ya siku 12 kati ya Iran na Israel.
Uhalisia wa Taarifa hiyo
JamiiCheck imefuatilia taarifa hiyo na kubaini kuwa taarifa hiyo inapotosha uhalisia.
Utafutaji kwa njia ya utafutaji wa maneno muhimu (keyword search) imebainika kuwa taarifa ama tukio hilo limekuwepo mtandaoni toka mwaka 2024 na si mwaka 2025 baada ya vita ya siku 12 kama ambavyo taarifa potoshi zinaeleza.
Tovuti ya JNS Disemba 16, 2024 iliripoti kuwa;
"Mwanaharakati wa upinzani wa Iran hivi karibuni alibadilisha jina la barabara moja huko Tehran kuwa la Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, “msafishaji wa uovu,” chombo cha habari cha London, Iran International, kiliripoti Jumamosi.
Haikufahamika mara moja ni wapi katika mji mkuu wa Iran alama ya barabara hiyo, ambayo ilionekana katika video iliyoshirikiwa na chombo hicho cha habari cha upinzani na “raia” asiyejulikana, ilitokea. Video hiyo ilionekana kuwa haina tarehe."
Hivyo video hiyo haihusiani na vita iliyotokea mwaka 2025 kati ya Israel na Iran