Ameutoa uhai wake kwa Watanzania!

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,605
12,230
Yeye ni Rais wa watanzania, wanyonge na hata matajiri. Lakini sio Rais wa matajiri. Mtu nilazima utafakari kabla yakupona.

Anaendelea kusema naomba mniombe kwa maana sito waangusha na anakwenda mbali nakusema ana amini ikiwa atafanya kazi vyema atakuwa mkuu wa Malaika kule mbinguni.

Huyo sio mwingine ila ni Rais wa Tano wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Huyu ni Rais wa aina yake ktk bara la afrika na kwa sasa Afrika nzima inataman japo huyu Rais aongoze mataifa yao japo kwa mwezi mmoja.

Mh Rais Dk John Pombe Magufuli ni rais wa aina yake ktk bara la afrika na zaidi sana ktk Taifa lake teule Tanzania.

MH Rais amekuwa mbele kuiona kesho yake nakujuwa kuwa Rais sio kuwa mpiga mipango nakula bata ikulu.

Amebeba maono ya uzalendo kwanza akiamini kuna maisha baada ya maisha haya na pia ipo taji kwa kuwa Rais mwaminifu kwa watu wake.
Mh Rais ameleta chachu ya maendeleo nakupambana na kila aina ya makandokando yanaifanya serikal ishindwe wafika watu wake.

Watu wengi hawamuelewi pale anaomba sala za watu na kusema amejitolea kwa watu wake, ila kiufupi anaitaji support yangu na yakwako wewe mtanzania kupambana na majangili wa rasilimali zetu.

Hii ni vita na kwa jinsi yeyote lazima tuishinde kwa vile Rais ametoa uhai wake kwetu na taifa ili tusonge mbele.

Ata sisi nilazima tutoe uhai wetu na kila tulicho nacho kutetea taifa letu. Nakwakufanya hvyo tunasonga mbele. Mungu ibariki Tz na Rais wetu. Amen
 
Mbona hiyo heading na contents za hiyo post zinatofautiana kwa mbali kama mbingu na nchi?
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Kweli imenenwa kuwa kupenda ni upofu.

Bunge limezuiwa kutoonyeshwa LIVE kwa sababu za 'kipuuzi' kabisa chini ya huyo huyo unayemshabikia.

Nchi haiendeshwi tena kwa Katiba wala kwa kutumia sheria nyinginezo chini ya huyo unayempenda kupindukia.

Nchi inaendeshwa kwa kile kitu kinachoitwa One Man Show, lakini bado wewe hulioni hilo.

Kweli nimeamini kwa apendaye hata kipofu atamwita ana makengeza............
 
Nchi yetu imeanza kutengwa na mataifa ya magharibi hadi kufikia kuanza kunyimwa misaada, kutokana na serikali ya awamu ya 5 kuiminya kwa kiasi cha kutisha Demokrasia, ina maana hata kwa hilo umejitia upofu na kujifanya hulioni hilo na badala yake umeamua kumpa bonge la Big up Magu!
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Bado sijaona jambo kubwa la kimageuzi ambalo amelifanya!Aviache vyombo huru viwe huru kweli,kama ameliminya bunge,ni nani atakayeisimamia na kuishauri serikali yake?
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Ukitaka tumuamini
Aache kudili na Sukari adili na maendeleo ya Nchi

Tunahitaji bunge live
Tunahitaji katiba ya warioba
Tunahitaji wale wote walio azimiwa na bunge kuwa wamepiga hela za escrwo akaunti wachukulie hatu
Tunahitaji kuona
Aongee kikatiba sio kila siku yuko kwenye tv tu
Tunahitaji

Aache mara moja tabiya ya kusema serekali ya magufuli

Katiba yetu inatambua serekali ya jamhuri ya mungano wa Tanzania
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Tunampenda na kumheshimu ni kiongozi wetu Magufuli ni Rais wetu , Mungu amlinde na kumuongoza vyema katika kazi zake za kila siku.
 
Ukitaka tumuamini
Aache kudili na Sukari adili na maendeleo ya Nchi

Tunahitaji bunge live
Tunahitaji katiba ya warioba
Tunahitaji wale wote walio azimiwa na bunge kuwa wamepiga hela za escrwo akaunti wachukulie hatu
Tunahitaji kuona
Aongee kikatiba sio kila siku yuko kwenye tv tu
Tunahitaji

Aache mara moja tabiya ya kusema serekali ya magufuli

Katiba yetu inatambua serekali ya jamhuri ya mungano wa Tanzania
Unamuhitaji Rais wenu Lowassa
 
Yeye ni Rais wa watanzania, wanyonge na hata matajiri. Lakini sio Rais wa matajiri. Mtu nilazima utafakari kabla yakupona.
Anaendelea kusema naomba mniombe kwa maana sito waangusha na anakwenda mbali nakusema ana amini ikiwa atafanya kazi vyema atakuwa mkuu wa Malaika kule mbinguni.
Huyo sio mwingine ila ni Rais wa Tano wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Huyu ni Rais wa aina yake ktk bara la afrika na kwa sasa Afrika nzima inataman japo huyu Rais aongoze mataifa yao japo kwa mwezi mmoja.

Mh Rais Dk John Pombe Magufuli ni rais wa aina yake ktk bara la afrika na zaidi sana ktk Taifa lake teule Tanzania.
MH Rais amekuwa mbele kuiona kesho yake nakujuwa kuwa Rais sio kuwa mpiga mipango nakula bata ikulu.
Amebeba maono ya uzalendo kwanza akiamini kuna maisha baada ya maisha haya na pia ipo taji kwa kuwa Rais mwaminifu kwa watu wake.
Mh Rais ameleta chachu ya maendeleo nakupambana na kila aina ya makandokando yanaifanya serikal ishindwe wafika watu wake.
Watu wengi hawamuelewi pale anaomba sala za watu na kusema amejitolea kwa watu wake, ila kiufupi anaitaji support yangu na yakwako wewe mtanzania kupambana na majangili wa rasilimali zetu.
Hii ni vita na kwa jinsi yeyote lazima tuishinde kwa vile Rais ametoa uhai wake kwetu na taifa ili tusonge mbele.
Ata sisi nilazima tutoe uhai wetu na kila tulicho nacho kutetea taifa letu. Nakwakufanya hvyo tunasonga mbele. Mungu ibariki Tz na Rais wetu. Amen
 
Yeye ni Rais wa watanzania, wanyonge na hata matajiri. Lakini sio Rais wa matajiri. Mtu nilazima utafakari kabla yakupona.
Anaendelea kusema naomba mniombe kwa maana sito waangusha na anakwenda mbali nakusema ana amini ikiwa atafanya kazi vyema atakuwa mkuu wa Malaika kule mbinguni.
Huyo sio mwingine ila ni Rais wa Tano wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Huyu ni Rais wa aina yake ktk bara la afrika na kwa sasa Afrika nzima inataman japo huyu Rais aongoze mataifa yao japo kwa mwezi mmoja.

Mh Rais Dk John Pombe Magufuli ni rais wa aina yake ktk bara la afrika na zaidi sana ktk Taifa lake teule Tanzania.
MH Rais amekuwa mbele kuiona kesho yake nakujuwa kuwa Rais sio kuwa mpiga mipango nakula bata ikulu.
Amebeba maono ya uzalendo kwanza akiamini kuna maisha baada ya maisha haya na pia ipo taji kwa kuwa Rais mwaminifu kwa watu wake.
Mh Rais ameleta chachu ya maendeleo nakupambana na kila aina ya makandokando yanaifanya serikal ishindwe wafika watu wake.
Watu wengi hawamuelewi pale anaomba sala za watu na kusema amejitolea kwa watu wake, ila kiufupi anaitaji support yangu na yakwako wewe mtanzania kupambana na majangili wa rasilimali zetu.
Hii ni vita na kwa jinsi yeyote lazima tuishinde kwa vile Rais ametoa uhai wake kwetu na taifa ili tusonge mbele.
Ata sisi nilazima tutoe uhai wetu na kila tulicho nacho kutetea taifa letu. Nakwakufanya hvyo tunasonga mbele. Mungu ibariki Tz na Rais wetu. Amen
 
Yeye ni Rais wa watanzania, wanyonge na hata matajiri. Lakini sio Rais wa matajiri. Mtu nilazima utafakari kabla yakupona.
Anaendelea kusema naomba mniombe kwa maana sito waangusha na anakwenda mbali nakusema ana amini ikiwa atafanya kazi vyema atakuwa mkuu wa Malaika kule mbinguni.
Huyo sio mwingine ila ni Rais wa Tano wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Huyu ni Rais wa aina yake ktk bara la afrika na kwa sasa Afrika nzima inataman japo huyu Rais aongoze mataifa yao japo kwa mwezi mmoja.

Mh Rais Dk John Pombe Magufuli ni rais wa aina yake ktk bara la afrika na zaidi sana ktk Taifa lake teule Tanzania.
MH Rais amekuwa mbele kuiona kesho yake nakujuwa kuwa Rais sio kuwa mpiga mipango nakula bata ikulu.
Amebeba maono ya uzalendo kwanza akiamini kuna maisha baada ya maisha haya na pia ipo taji kwa kuwa Rais mwaminifu kwa watu wake.
Mh Rais ameleta chachu ya maendeleo nakupambana na kila aina ya makandokando yanaifanya serikal ishindwe wafika watu wake.
Watu wengi hawamuelewi pale anaomba sala za watu na kusema amejitolea kwa watu wake, ila kiufupi anaitaji support yangu na yakwako wewe mtanzania kupambana na majangili wa rasilimali zetu.
Hii ni vita na kwa jinsi yeyote lazima tuishinde kwa vile Rais ametoa uhai wake kwetu na taifa ili tusonge mbele.
Ata sisi nilazima tutoe uhai wetu na kila tulicho nacho kutetea taifa letu. Nakwakufanya hvyo tunasonga mbele. Mungu ibariki Tz na Rais wetu. Amen
Kwenye heading nilijua amejiua kama Mkwawa..!
 
Kweli imenenwa kuwa kupenda ni upofu.

Bunge limezuiwa kutoonyeshwa LIVE kwa sababu za 'kipuuzi' kabisa chini ya huyo huyo unayemshabikia.

Nchi haiendeshwi tena kwa Katiba wala kwa kutumia sheria nyinginezo chini ya huyo unayempenda kupindukia.

Nchi inaendeshwa kwa kile kitu kinachoitwa One Man Show, lakini bado wewe hulioni hilo.

Kweli nimeamini kwa apendaye hata kipofu atamwita ana makengeza............
Lipo tbc 2 linaonyeshwa
 
Yeye ni Rais wa watanzania, wanyonge na hata matajiri. Lakini sio Rais wa matajiri. Mtu nilazima utafakari kabla yakupona.
Anaendelea kusema naomba mniombe kwa maana sito waangusha na anakwenda mbali nakusema ana amini ikiwa atafanya kazi vyema atakuwa mkuu wa Malaika kule mbinguni.
Huyo sio mwingine ila ni Rais wa Tano wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Huyu ni Rais wa aina yake ktk bara la afrika na kwa sasa Afrika nzima inataman japo huyu Rais aongoze mataifa yao japo kwa mwezi mmoja.

Mh Rais Dk John Pombe Magufuli ni rais wa aina yake ktk bara la afrika na zaidi sana ktk Taifa lake teule Tanzania.
MH Rais amekuwa mbele kuiona kesho yake nakujuwa kuwa Rais sio kuwa mpiga mipango nakula bata ikulu.
Amebeba maono ya uzalendo kwanza akiamini kuna maisha baada ya maisha haya na pia ipo taji kwa kuwa Rais mwaminifu kwa watu wake.
Mh Rais ameleta chachu ya maendeleo nakupambana na kila aina ya makandokando yanaifanya serikal ishindwe wafika watu wake.
Watu wengi hawamuelewi pale anaomba sala za watu na kusema amejitolea kwa watu wake, ila kiufupi anaitaji support yangu na yakwako wewe mtanzania kupambana na majangili wa rasilimali zetu.
Hii ni vita na kwa jinsi yeyote lazima tuishinde kwa vile Rais ametoa uhai wake kwetu na taifa ili tusonge mbele.
Ata sisi nilazima tutoe uhai wetu na kila tulicho nacho kutetea taifa letu. Nakwakufanya hvyo tunasonga mbele. Mungu ibariki Tz na Rais wetu. Amen

Kwa ajili ya usalama wangu na ustawi wa familia yangu ngoja nijaribu kuchangia bandiko hili kwa tahadhari ili nisijikute nimetupwa korokoroni,maana wakati zinapitishwa sheria za uharifu wa kimtandao,hatukujua kama yalikuwa ni maandalizi ya kuelekea kwenye giza la upatikanaji wa habari.

Mleta mada kwa makusudi au kwa kujitoa ufahamu,unajaribu kumvika mtu sifa za utukufu asionao.Kumbuka unayejaribu kumvika utukufu hajashushwa toka mbinguni,alikuwa ni sehemu ya serikali za awamu mbili zilizopita,ambazo kwa kiasi kikubwa,ndizo zilizolifikisha Taifa hili katika mkwamo huu tulionao.Alikuwa sehemu ya Baraza la mawaziri katika awamu ya tatu,na akarejea katika Baraza la mawaziri la awamu ya nne.

Chini ya utumishi wake katika ofisi alizopewa dhamana ya kuzisimamia,yapo mengi mazuri aliyoyafanya,lakini naye kama walivyo wanadamu wengine,alifanya mambo mengi ambayo hadi leo bado Taifa halijapona makovu ya maamuzi yake kama kiongozi,sina sababu ya kuyataja hapa kwani yapo wazi na yanajisimamia yenyewe bila kuhitaji kurunzi hata usiku wa giza.

Tunabahati kama Taifa kuongozwa na serikali ya chama kimoja toka tutoke mikononi kwa wakoloni.Tunayoyapitia na kuyashuhudia leo ni kielelezo cha kushindwa kwa serikali ya chama cha mapinduzi,uozo ulioligubika Taifa ni matokeo ya utawala ulioshindwa wa ccm,ni ccm iliyoasisi na kusimamia kila uovu ambao leo hii wapumbavu wa aina yako wanaona fahari kwa kudhani shetani yule aliyelikandamiza Taifa letu,sasa amebadilika na kuwa malaika.

Wenye hekima walitufundisha kuwa" hatuwezi kuyatatua matatizo yetu kwa kutumia njia zilezile zilizotufikisha hapa tulipo".Hata wenye chama chao walishatuambia kuwa ccm ni ileile,lakini kwa sababu ya ujinga wetu,tulishiriki kuitikia wimbo uliobeba maonyo,sisi tukaugeuza burudani.

Hebu toka hadhalani,jivue joho la itikadi za vyama na ulitazame Taifa letu kwa upendo,si hawa unaowapa utukufu ndiyo waliotufikisha hapa?Unakumbuka mabilioni ya shilingi yaliyopigwa katika wizara ya ujenzi katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu?Una ufahamu wowote kuhusu hasara tulizozipata kama Taifa kwa kulipia fidia zilizotokana na maamuzi ya huyo "mtakatifu wako?Unakumbuka namna Taifa linavyotumia mabilioni ya shilingi kulipia nyumba za watumishi wake ilihali Taifa hili lilikuwa na nyumba za kutosha lakini " mtakatifu wako aliyejaa upako" alisimamia mauzo ya NYUMBA hizo na zingine zikatolewa Zawadi kwa "mababy mamaz?"

Sitaki niwe mtoa hukumu,lakini kama dhamira ya ccm na serikali zake ilikuwa ni kuleta ustawi wa Taifa letu,ilikuwaje ccm hiyo hiyo ikaruhusu kila aina ya uchafu na ufisadi ukatamalaki nchini?Escrow,kagoda,Richmond,mabehewa feki,kivuko kibovu,uuzwaji wa nyumaba za serikali,Rada na ndege ya rais,haya yote yalifanyika chini ya serikali hii sikivu ya ccm tena kwa maapizo ya kidharimu ya "bora Watanzania tule nyasi,lakini ndege ya rais inunuliwe". Kama mtakatifu wako ana nia njema na Taifa hili,alipaswa aanze kuwawajibisha watangulizi wake,hasa yule aliyefungua biashara ikulu kwa kusajili kampuni ya ANBEN,kitendo cha kutimuwajibisha kwa uharifu alioufanya wa kuivunja katiba aliyoapa kuilinda,kimemfanya atuone Watanzania ni malofa na wapumbavu.

Ni Tanzania pekee ambako mbele ya usalama wa Taifa na vyombo vyote vya serikali,watu waligawana mabilioni ya shilingi na kuyapakia katika mifuko ya Rambo na kutokomea pasipojulikana.Hivi mtakatifu wako anashindwa nini kulitumbua jipu hili la Escrow ambalo lilishaiva kitambo? Au ameshikwa kigugumizi kwa kuwa shehena hiyo iliyopakiwa kwenye Rambo na sandarusi ilifika hadi ikulu ya mkwele na kupokelewa na mnikulu wake ndugu Gulumo?

Upumbavu wa mleta mada na wenzake waliojipanga kuitikia pambio za #HapaKaziTu,badala ya kuhoji waliolifikisha Taifa letu hapa tulipo wamechukuliwa hatua gani,ni kielelezo cha mwisho cha nakisi ya ubongo tuliyonayo Watanzania.Ni Tanzania pekee ambako viongozi mkuu wa wizara anatoa agizo la kuzimwa flowmeter zinazopima kiasi cha mafuta kinachoingizwa nchini,anahujumu mapato ya Taifa lakini analindwa na badala yake anatumbuliwa mtu wa chini aliyetekeleza agizo la bosi wake na bado watu wa jamii ya mleta mada wapiga kelele za kusifu na kuabudu serikali.

Tufike mahali tuache itikadi zetu,tuwe macho kudai haki zetu,ni kupitia madai yetu tu ndiposa serikali hii ya watu wale wale waliyoyatengeneza matatizo tuliyonayo,inaweza kusikia kishindo cha kilio chetu na kutimiza wajibu wake,vinginevyo tutawafanya wazidi kutuona malofa na wapumbavu kwa kushindwa kwetu kuuona Ukweli wa namna Taifa lilivyogegedwa na magegedu hawa ambao leo tunawaimbia nyimbo za sifa.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!!!!.
 
Hivi yule wanayemuitaga Rais wa mioyo ya watu yupo wapi aiku hizi? Hatakuja kukanyaga Chato mpaka anaingia kaburini
 
Nchi yetu imeanza kutengwa na mataifa ya magharibi hadi kufikia kuanza kunyimwa misaada, kutokana na serikali ya awamu ya 5 kuiminya kwa kiasi cha kutisha Demokrasia, ina maana hata kwa hilo umejitia upofu na kujifanya hulioni hilo na badala yake umeamua kumpa bonge la Big up Magu!
Una uhakika na ulichoandika?
 
Back
Top Bottom