American colonialism | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

American colonialism

Discussion in 'International Forum' started by Ami, Aug 22, 2011.

 1. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ukoloni mpya umeingia duniani ambapo taifa lenye nguvu za kijeshi na linalopungukiwa nguvu za kiuchumi linazidi kutanua makucha yake.
  Tayari wana makoloni katika central Asia ambayo ni Afghanistan na Pakistan.Kwa upande wa mashariki ya kati wamekuwa na vikoloni viwili kwa muda ambavyo ni Kuwait na Qattar huku ikijiimarisha kwenye koloni lake jipya la Iraq.
  Kwa Afrika wamechagua koloni lenye utajiri mkubwa wa mafuta ambalo ni Libya.Kupitia Libya inatarajiwa nguvu kubwa itapatikana kuzitawala nchi zote za Afrika na mashariki ya kati.
  Tofauti na ukoloni mkongwe ambapo udhaifu wa mababu uliwezesha kutawaliwa kirahisi kupitia hadaa kama za kuoneshwa sura yake mwenyewe mtu kwenye kioo.Ukoloni wa sasa unatumia teknolojia ya habari na silaha za maangamizi kuwatisha na kuwauwa wababe hata kama wana elimu na teknolojia kuliko mababu wa enzi zile.Kwa upande mwengine mpira wa miguu na sinema vimekuwa viota madhubuti vya kuzalisha mazuzu yanayounga mkono ukoloni huu mpya kama wanavyoonekana maeneo mbali mbali Afrika na mashariki ya kati.

   
 2. K

  Kidzude JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 2,727
  Likes Received: 332
  Trophy Points: 180
  Tupo wote lakini umetunyima jani. Fafanua zaidi juu ya kupata masoko kupitia culture ,, Music Lugha michezo na etc. Tupe mwongozo jinsi ya kutumia vyombo vya habari kututrick. Sema ni namna gani waweza ingizwa mkenge na western kama uswahiba savimbi etc.
   
 3. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #3
  Aug 22, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Ilo jani safari hii Ami kaamua kulivuta peke yake!
   
 4. Mr.Toyo

  Mr.Toyo JF-Expert Member

  #4
  Aug 22, 2011
  Joined: Feb 9, 2007
  Messages: 433
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  No comment... :)
   
 5. ATUGLORY

  ATUGLORY Senior Member

  #5
  Aug 22, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ami


  UNLESS YOU BACK UP YOUR ASSERTIONS WITH TANGIBLE AND REALISTIC EVIDENCE, i CAN ONLY DISMISS YOUR THREAD AS ONE OF THOSE LIBERAL/LEFT LEANING AND UNSUBSTANCIATED CONSPIRACY THEORIES, AU LABDA UNA AGENDA ya SIRI UNAYOIFICHA BETWEEN THE LINES, VINGINEVYO TUELEZE AMERICA WAMECOLONIZE VIPI PAKISTANI, ZAIDI YA UKWELI KWAMBA WAKO HUKO KUTAFUTA MAGAIDI, au tueleze kama una Conflict of Interest na Agenda ya Ugaidi!ambayo moja ya malengo yake ni kuiona America iliyoodhoofika ili kutimiza malengo ya kugaidi ya kuingiza ukoloni wa kidini kupitia alqaeda??!!! Halafu kuna Tatizo gani kama serikali halali ZA Kuwait na QATAR Zimeamua kukaribisha taifa "Rafiki" la MAREKANI KUWEKA MILITARY BASE KWENYE NCHI YAO WEWE MSWAHILI INAKUUMA NINI!!!????
   
 6. quimby_joey

  quimby_joey JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 361
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Nakabuliana na wewe kwa asilimia zote, kwanini nguvu hizi hazijaelekezwa somalia, Syria na hata sudan kusini? wamefanikiwa
   
 7. K

  Kidzude JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 2,727
  Likes Received: 332
  Trophy Points: 180
  Mheshimiwa Atu Ungetoa hint ya nini mtoa mada anatakiwa kutueleza maana hii ni moja ya makala ndefu sana ambayo inatakiwa kutolewa kwa big thinkers. labda haitakiwi kujadiliwa humu.
   
 8. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #8
  Aug 22, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Jani lenyewe ni kama yale yanayotokea Libya jana na leo.Ambalo nilisahau kabla ni hizi chaguzi za kidemokrasia na kuunga mkono tawala za kifalme.
  Wale wafalme wote wa mashariki ya kati kama si watoto wa marafiki za Marekani na UK basi wenyewe wamesoma huko huko wakabadilishwa bongo zao.Mambo hayajaenda sawa kwa Bashar Al Assad tu ambaye ndiye next target kabla ya mkakati mkubwa zaidi dhidi ya Iran baada ya ule wa uchaguzi wa mwaka juzi kupitia tweeter kusambaratika
  .
   
 9. s

  sanjo JF-Expert Member

  #9
  Aug 22, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  American colonialism on the pretext of preserving human rights is great for the most downtrodden people. Fikiria Gadhafi & family, Sadam Hussein & Sons, Mubarak & Family etc, je ni halali kwa watu kama hao kujifanya wamiliki wa kila kitu katika nchi zao?
   
 10. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #10
  Aug 22, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,050
  Likes Received: 3,080
  Trophy Points: 280
  Ami umegusa maeneo nyeti ya kisayansi ya ukoloni mpya japo wengine bado hawajakupata,katika hali kama hii ambayo mafuta,madini na vyanzo vingine vya uchumi vinaonekana kuhitajika na kila nchi,Marekani yenyewe inatumia ukoloni wa kisayansi wa kusaidia vita,kusaidia kupambana na maradhi,kutoa uduma za kibinadamu huku wakizidi kuingiza sera zao karibu katika kila nchi k2 ambacho wamefanikiwa

  Tofauti na wenzao walioonekana kutumia sana mabavu enzi za nyuma wao mabavu ni sehemu ya mwisho lakini mwanzo wanatengeneza mazingira ya wewe kuingia mwenyewe huku wakitumia pesa kidogo kupata nyingi,wakitumia vyombo vya habari kuvutia na kuharibu uwezo wa vijana kufikiria e.g bongo fleva,na kuvaa nusu uchi ili wapate kufanya kitu kinaitwa cultural imperialism

  Tumekubali kutawaliwa kiteknolojia na kisomi na sera za maendeleo zinapangwa NY city
   
 11. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #11
  Aug 22, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kabisa!,Rweye.
  Jengine ni kila nchi kulazimishwa kuwa na wizara ya wanawake na watoto.Hii wizara ni moja ya vipenyo vya kupata watu mazumbukuku ya kuunga mkono ukoloni huu mpya.
  Muda umefika wa kila kiongozi kuja na sera zake ili tupime akili yake.Tungekuwa na maraisi angalau watatu kama yule bedui-Ghadafi mambo ya dunia yasingekuwa kama sasa ambapo watu wanaoitwa wasomi hutumia ujinga kutawala raia zao.
   
 12. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #12
  Aug 22, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  dah! Inauma sana kuona tunatawaliwa mchana mbuzi anakula majani mie mzungu akiingia anga zangu NAMUUA
   
 13. K

  Kidzude JF-Expert Member

  #13
  Aug 22, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 2,727
  Likes Received: 332
  Trophy Points: 180
  Mzee mbona unatuingiza choo sicho. Wizara ya wanawake na watoto na bedei gadafi zinahusiana vipi na kichwa cha mwongozo wako. Aisee mi natoka nje ya ukumbi sasa unless uombe radhi. La sivyo nitatumia ur facial expression ku kujudge otherwise.
   
 14. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #14
  Aug 24, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Former Belgian MP: "Second colonization of Africa underway"
  Africa is about to become the victim of the second big colonisation grab -- this time with the whites using massive bombs and fire-power, massacres and plunder without risk of losses to the coward racists hiding behind their machines, unconscious slaves to the money-men
   
 15. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #15
  Aug 24, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Hapo ndo wakati mwingine huwa najiulizaga kama aidha swaumu imekuzidi mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani au labda kama sio hivyo basi umekula msuba wa Kitonsa. Manaake fikra zako zinanichanganya!
   
 16. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #16
  Aug 25, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kuna jamaa alikuwa anamshutumu Askari kanzu kuwa yupo kwenye payroll ya wakoloni.Ikiwa ni hivyo huenda muko pamoja.
  Inatia shaka kwamba baadhi yenu munaelewa facial expressions zetu kiasi hicho hata munatishia kuzitumia kutuanika.
  Ukiangalia topic za Askari na jinsi ambavyo nyengine zote zinachanganywa kwake ili zisianguke utajuwa hiyo hali.
  Akina Muhadhiri wamechoka wakajiondoa kwa hofu kwamba hili ni jukwaa linalogharamiwa na wakoloni kuendeleza ukiritimba.Asanje ametutonya tayari.
  Mimi bado nipo ikiwa sitoonekana nuksi kwa wakoloni nikabughudhiwa kama akina Malaria na Faiza.Nipo kwa vile kama Mrema naamini sikuzaliwa nikiwa na JF.
   
 17. K

  Kidzude JF-Expert Member

  #17
  Aug 25, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 2,727
  Likes Received: 332
  Trophy Points: 180
  Sorry kama nimekuudhi. Lakini unapochangia usionyeshe element fulani ambazo watu watakudge vinginevyo. ''Wizara ya wanawake na watoto"' hii inaleta maana gani. Askari kanzu nimepishana nae kwa sababu tu ni kuwa nae pia ana msimamo ambao umeegemea kwenye mtazamo fulani ambao wewe na yeye hamuwezi katu kukaa pamoja. Pia naweza kuwa na msimamo na wewe wa mambo fulani lakini si kwa sababu zinazofanana. Ili uweze kuchangia vema yapasa utoe hisia zozote ambazo kama utaziweka hadharani zitaleta shida. i.e UDINI, UKABILA UKANDA AU KIPATO.
   
 18. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #18
  Aug 25, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hivyo vitu na vyengine hukuvitaja kwa mfano ujinga,uchoyo,uroho kinyongo,kiburi,ubarakala.......
  Mara nyingi huwa tunaonyana kuviwacha lakini si rahisi kwangu, kwako,kwa Askari na kwa JF.Kila mmoja huwa ameathiriwa na kimojawapo au zaidi.Binafsi sivipendi lakini najuwa sina namna ya kuvizuia.Vyengine vina tiba na vyengine ni sugu kwa baadhi ya watu. Na wewe sina shaka huwezi kuonesha mfano kuwacha kile kinachokuathiri.Nikukusoma kidogo tu nitakuleza ukoje.Ukiniangalia mimi utagundua nimeathiriwa na kipi kati ya hivyo.
  Mambo yanayotokea Libya na Iraq ni uroho na udini.Kule Gaza ni kiburi cha Israel chenye chembe za udini.Hapa JF ni ukabila na udini kwa upande wa member.Kwa uongozi kutakuwa na mengine. Si rahisi kumshawishi Askari kanzu akaamini kuwa Ghadafi ni mwafrika.Ujinga nao unawafanya baadhi yetu tusione kwamba Libya inakaliwa na binadamu kama sisi.
  Kwa hayo Kidzude utapata tabu kulazimisha kuyaondoa na kunyoosha michango yetu isioneshe hisia zake........
  falsafa za Ami
   
 19. K

  Kidzude JF-Expert Member

  #19
  Aug 25, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 2,727
  Likes Received: 332
  Trophy Points: 180
  Mzee noted and saved for future reference. Hayo yoote ni mambo ambayo yanatufanya tutofautiane. Mwisho ni kukubali kutokubalinana na maisha yakasonga.
   
 20. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #20
  Aug 25, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kuna ukoloni wa kila aina siku hizi kuanzia hiyo Amercan colonialism ulioisema hadi Arab colonialism.
  Nakushauri ufuate yafuatayo ili kufanikisha fikra zako:
  1. Waeleze wenye Bureau de Changes wasifanye transactions za sarafu ya US Dollar $$
  2. Kama una American products nyumbani uzitupe jalalani mfano Dell computers/laptops, Apple/HP computers, iPhones, iPads, Cisco phones etc.
  3. Waambie watanzania waache kwenda kuomba visa pale American embassy
  4. Vituo vyote vya TV viache kurusha vipindi vya kimarekani kama House, ESPN, CNN, CSI-Miami, NY etc
  5. Majumba yote ya sinema yasionyeshe movies za Holywood, waonyeshe picha za kichina, Russia, Middle East etc
  6. Watu waache mara moja kunya Coca cola, Fanta, Pepsi, burgers etc
  7. Madisco yasipige Hip hop music
  8. Fanya juhudi JK aufunge ubalozi wa marekani hapa Tanzania na tusiwe na uhusiano wa aina yoyote na USA
  9. Waambie watanzania na wazanzibari wote wlioko US waondoke na kurejea bongo mara moja
  10. Acha kutumia internet wala kutuma e-mails usiingie kabisa ktk mitandao kama Yahoo, google, msn etc
  Na mengineyo mengi tu
   
Loading...