Amenipimisha HIV kisha amekata mawasiliano

boyson onlye

JF-Expert Member
Sep 13, 2015
1,103
1,382
Ni week kadhaa sasa zimepita tangu nitimize sharti lake moja lililobaki ili niingie rasmi kwenye mahusiano ambayo nimeyapigania karibia mwaka sasa, tangu aje jiji dsm kutokea mkoa M, alifikia kwa dada baadae akapata kazi shule flani ya magar ya njano hapa mjini, mda huo wote nilikuwa na nawasiliana nae na nilishamwelezea hisia zangu, akaniambia hayuko kuingia kwenye mawasilaino nikajikuta amenifanya friend for benefit ila sikujali hilo kwa kuamini kuwa siku moja hapa ndipo nitapumzisha moyo wangu kwa sababu nilashaamua na safari yetu ya kuanzisha familia nitaanza naye huyu bint

Siku zikapita na bado tunawasiliana mambo mengi tukishirikishana hatimaye siku moja akaniiita dinner mahali flani wanapouzaga yule mdudu anayepigwa vita, wakati tunasubiri yule mdudu aivishwe kwa sababu wote hatutumii alcohol, tukiendela na soft drink nikapokea taarifa ambazo usiku ule niliuona wenye faraja sana kwangu, aliniambia J nimekaa nimefikilia nimeona ukitaka tuingie kwenye relationship twende tukapime kwanza, nikamwambia usijali, tukapanga siku ya kwenda kupima ile siku ilipofika akaniambia anadharula, mimi nikasema siyo kesi kwa sababu yeye anawasiwasi na mimi wacha niende mwenye,
japo ki ukweli nikawa nawaza ya nyuma kirho kinaniambia nipotezee ila nikimuwaza huyu mtoto nikajisemea moyoni liwalo na liwe, nikazama zangu hosp moja hivi mjini nikaongea na doctor kuwa nimekuja kuchek HiV wakaniuliza maswali yao fresh nikacheeki na majibu yakatoka, Furaha ikaongezeka kwa sababu yametoka fresh, nikampigia simu nikamweleza akaniambia sawa subiri tukacheki wote next time,

wakuu tangu nimweleze majibu na amekata kabisa mawasiliano, message hajibu tena hata simu hapokei
wazoefu niambie nimekuwa na kiherehere cha kupima hivyo ka mind or

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We umemuwahi anahisi kuna kamchezo utakua umemchezea rafu ila usijali atarudi Tu na yeye anataka akapime kwanza kabla hamjaenda wote asa ukiona kimya kingi ujue kashapima af jiongeze sababu anakupenda
 
Write your reply...bwana ametoa bwana ametwaa jina lake lihiidimiwe mbele yako nyuma yetu mwangaza wa milele ukuangazia katika makazi yako mema

samahan haya niliyoandika hayaendani na mada wala msinifikirie vibaya najifunza Ku type hapa naperuzi jf kutumia desktop

nikirud mkuu nitakupa ushauri
 
Ni week kadhaa sasa zimepita tangu nitimize sharti lake moja lililobaki ili niingie rasmi kwenye mahusiano ambayo nimeyapigania karibia mwaka sasa, tangu aje jiji dsm kutokea mkoa M, alifikia kwa dada baadae akapata kazi shule flani ya magar ya njano hapa mjini, mda huo wote nilikuwa na nawasiliana nae na nilishamwelezea hisia zangu, akaniambia hayuko kuingia kwenye mawasilaino nikajikuta amenifanya friend for benefit ila sikujali hilo kwa kuamini kuwa siku moja hapa ndipo nitapumzisha moyo wangu kwa sababu nilashaamua na safari yetu ya kuanzisha familia nitaanza naye huyu bint

Siku zikapita na bado tunawasiliana mambo mengi tukishirikishana hatimaye siku moja akaniiita dinner mahali flani wanapouzaga yule mdudu anayepigwa vita, wakati tunasubiri yule mdudu aivishwe kwa sababu wote hatutumii alcohol, tukiendela na soft drink nikapokea taarifa ambazo usiku ule niliuona wenye faraja sana kwangu, aliniambia J nimekaa nimefikilia nimeona ukitaka tuingie kwenye relationship twende tukapime kwanza, nikamwambia usijali, tukapanga siku ya kwenda kupima ile siku ilipofika akaniambia anadharula, mimi nikasema siyo kesi kwa sababu yeye anawasiwasi na mimi wacha niende mwenye,
japo ki ukweli nikawa nawaza ya nyuma kirho kinaniambia nipotezee ila nikimuwaza huyu mtoto nikajisemea moyoni liwalo na liwe, nikazama zangu hosp moja hivi mjini nikaongea na doctor kuwa nimekuja kuchek HiV wakaniuliza maswali yao fresh nikacheeki na majibu yakatoka, Furaha ikaongezeka kwa sababu yametoka fresh, nikampigia simu nikamweleza akaniambia sawa subiri tukacheki wote next time,

wakuu tangu nimweleze majibu na amekata kabisa mawasiliano, message hajibu tena hata simu hapokei
wazoefu niambie nimekuwa na kiherehere cha kupima hivyo ka mind or

Sent using Jamii Forums mobile app

Sasa kama hili litapita basi chukua somo hapo. Wakati mwingine huwa nawambia ninaokutana nao kwamba kuna sheria, kanuni ama taratibu ambazo hujaridhia moja kwa moja wala kusign kwamba utafuata utekelezaji wake ila zina nguvu kuliko hata mikataba ya kwenye makaratasi.
Hii ni kwa sabau kitendo umekiuka utaratibu huo ama kanuni, hukumu ama madhara yake unayaona hapohapo na yanabeba taarifa nyingi kuhusu wewe ambazo hukuwahi kutoa maelezo.

Nakunukuu: "aliniambia J nimekaa nimefikilia nimeona ukitaka tuingie kwenye relationship twende tukapime kwanza" mwisho wa kunukuu.
Hapo ukiangalia kauli yake ilikua inahitaji upimaji ufanyike katika uwepo wenu wawili. na hapo ishu ilikua sio majibu tu bali ni yeye kushuhudia tangua mnaondoka, manapokua njiani, mudi yako njiani na wakati wa kusubiri majibu, na pia pale majibu yanapokua yanaanza kutolewa.

Kinyume chake wewe umefanya haya: nakunukuu; "nikazama zangu hosp moja hivi mjini nikaongea na doctor kuwa nimekuja kuchek HiV wakaniuliza maswali yao fresh nikacheeki na majibu yakatoka," mwisho wa kukunukuu.
Hapo umejitenga tayari ukahisi shida yake ilikua ni majibu. Vipi kama ulitengeneza majibu? Hapa ameona pengine hujiamini na ndio maana ukajiwahi fasta. Hukua na ujasiri wa kutosha kumruhusu yeye kushuhudia majibu yako. Sasa maamuzi yake yanaweza kua ya muda, akarudi baada ya kutafakari ama asirudi kwa sababu jaribio la kwanza na rahisi na linalohitaji umoja na mshikamano na kujiamini limekushinda.

Jipange upya ila wakati mwingine, usirudie hili kosa na mengine yafananayo na hilo. kwenye hizi hatua za mwanzo unahitaji kuwa makini haswa na kusikiliza kwa makini kuliko kawaida, kosa moja tu linaweza kukutoa ulingoni halafu ukute wanaotafuta usajili hapo ni foleni, wewe unakua ushapoteza nafasi ya mchujo wa awali.

Hata hivyo, huku kupima mapema hivyo manataka kufanyaje? maana hata mahusiano yenu yanaonekana bado machanga. Nia yako ovu ndio pengine imesitisha hilo zoezi. Tafuta hela kwanza acha kutumia nguvu bila manufaa.

Ahsante
 
Back
Top Bottom