Ameniomba nimvishe pete

Tushfutshtar

Senior Member
Joined
Dec 30, 2017
Posts
117
Reaction score
112
Hello! JF members,

Bila shaka hamjambo sana na kwa wale wenye changamoto tuzidi kumtegemea Mwenyezi Mungu na kujibidisha katika kujijenga.

Kama kichwa cha habari kisemavyo , juzi kati nilikuja na uzi wenye kichwa kilichosema "Tumekutana WhatsApp tukapendana haswa!" kwa kweli maendeleo yetu ni ya hali ya kawaida licha ya kuwepo minato (usumbufu) fulani wa kimahusiano, hasa kutoka kwa mwenzangu huyu wa kike! Ni mambo ya kawaida katika mahusiano. But all in all ni kuwa amenambia nimvishe Pete !

Sio kwamba sifahamu pete maana yake ni nini, na ni kwa lengo gani lakini alama yangu ya kujiuliza ipo kwenye "yeye mwenyewe kuomba nimvishe pete" sasa naomba kwa wale walio na uzoefu na haya mambo je hii nayo ni sehemu na haki ya mpenz kuomba kuvishwa Pete ? Je italeta maana halisi ya pete ikiwa ni pete ya kuomba avishwe! Au ni mtego fulani anataka anikamate mapema kabla sijamshtukia japo anadai hii ndo itampa uhakika kwamba niko serious na mahusiano! Najiuliza mwenyewe je yote nayofanya kwake mahitaji ya kimahusiano haoni kama ni upendo kweli hadi nimvishe pete?

Naomba wazorefu mnipe hints hapa, tafadhali, (sio wote) kwa wale wa kukebei kama huna kuchangia is better ukatunza mda wako, chaji ya simu yako na kufanya kazi zingine kuliko ku comments negatively.
 
ndo naanza kuona kwako mtu ana force kuvishwa pete..

dunia haishiwi viroja.

mna muda gani kwenye mahusiano kwanza????
 
Najuaga hayo mambo huja yenyewe hayaombwi

Upendo wa kweli hauoneshwi kwa kuombwa kuvishwa pete, ni jinsi wenyewe mnavyoishi kwa kujikomit kwenye mapenzi yenu

Kama unaona huo ni mtego bas jihadhari nao, usimvishe halaf uone atakavyokua anaact kwako
 
Najuaga hayo mambo huja yenyewe hayaombwi

Upendo wa kweli hauoneshwi kwa kuombwa kuvishwa pete, ni jinsi wenyewe mnavyoishi kwa kujikomit kwenye mapenzi yenu

Kama unaona huo ni mtego bas jihadhari nao, usimvishe halaf uone atakavyokua anaact kwako
Ahsante madame s, ngoja nitafakari ikiwa sitamvisha atachukuwa hatua gan! Ahsante sana!
 
nijuavyo mimi kumvisha mtu pete haimaanishi kama ndo unamuoa... ndoa ni kitu kingine cha umuhimu mvishe kama anavyotaka hata akitaka mpaka miguuni mvishe tu... ila kuwa makini sana mademu wa whatsapp kwenye magroup humo wamepita sehemu mbali mbali sana na wengine hata mtungo washafanyiwa... nimesema tu.. 🙂
 
Mwanamke hata mkikutana kanisani kwa vile hujui historia yake ni wa kuacha tu walivyo...wapo watu walikuwa Malaya wa kujiuza na siku ukimkuta kanisani utasema huyo ndio sasa kumbe choka mbaya
 
Mwanamke hata mkikutana kanisani kwa vile hujui historia yake ni wa kuacha tu walivyo...wapo watu walikuwa Malaya wa kujiuza na siku ukimkuta kanisani utasema huyo ndio sasa kumbe choka mbaya
mkuu kama umempata kwenye magroup ya whatsapp em jiulize haya:
1. anawezaje kukupenda kwa kuangalia picha yako tu na akakuweka moyoni.

2. mazingira yanayomzunguka ana wanaomwona wangapi na kwann wasimtetemekee wakamwacha kama alivyo.

3. kama ameweza kukukubalia wewe bila kukuona kuna wangapi alishafanya kama kwako...

4. kwann anataka kuonyesha upendo wa hali ya juu wakati penzi bado changa.. anataka usigundue kitu gani na ukigundua uwe tayari ushafunga ndoa...

fikiria sana kijana mtandaoni kuna vioja sana humo....
 
Umenikumbusha mbali sana huo mtungo.

adolescence [emoji38][emoji38][emoji38]
 
Pete Ni Nini?
Pete Ni Aina Flani ya Kitu chenye Umbo la Mduara Ambacho hutumika Kwa matumizi mbali mbali

Mfano.
Kusafishia Nyota, Kwa Wanandoa , kutumika kama hirizi, Nk.

___Ushauri___ Mvalishe ,wewe siyo Wa Kwanza wenzako Tulishatoa Na Mahari Kabisa Tulivyoona Sikio Linazidi Kichwa Tukala Kona. Sembuse Pete Tu.

@m G00d Br0ther
 
Kwani shida iko wapi??
Nenda kwa chinga chagua pete ya jero mvishe hafu sepa
 
Mimi nimeoa nina mwaka wa tano huu na sijui pete imekaaje. Mara baada ya ndoa mama watoto wangu alinunua pete 2 nzuri akanipa moja nivae, ndani ya wiki sijui hata zilipotelea wapi. Mambo ya wazungu haya sisi wapi na wapi @Tushfutshtar mkuu wewe endelea kuchunguza tu kwanza na huku ukisema na moyo wako, watoto wa kwenye mitandao hawa wana tabu sana kuwa makini mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…