Amenichumbia lakini hataki Ndoa

Ukilipiwa mahari au barua ya uchumba tayari ushaolewa, kulipiwa mahali ni sawa na kuolewa kimila, ukitaka funga ndoa ya serikali nayo ina makaratasi, ya kanisani ina makaratasi na inagharama, kama hana utayari wa harusi ndio imetoka hio ni ndoa kama unaamini kwenye harusi zaidi achia ngazi mapema.
 

Yumo humu pia ukawa unauliza humu na maelezo kiuwazi hivyo!!!!! Sasa na mtoto anakuja, tulia na usali.
 
Bomani kwani hawana dini hao?! Makanisani na misikiti wanafungisha ndoa za kimya kimya bila kelele tena siku za kazi katikati ya wiki,ni wewe tu na mwenzako kujiandaa kwenda na mashahidi wenu. Ndoa chap mnarudi kuendelea na maisha ya ndoa.
 
Ajutie kwa kipi labla nimeandika kwenu umefukuzwa we umeelewa vipi naona unanishutumu yaani bibie kurudi kwao ata jutia inashangaza hajaolewa why ajutie kurudi kwao, yes arudi kwao ili kama Mwanaume kama ana nia kweli amuoe sio anafaidi tunda kufata utamaduni na mila hataki.
 
Wasiwasi Ndiyo Akili Japo Ukweli Sisi Wagalatia Mambo Ni Mengi Sana Ila Sijajua Upande Dini Ya Mudi Mambo Ni Rahisi
Chukua Hatua Lazima Lipo Jambo Tu
Napenda Baada Ya Ushauri Jitahidi Uje Baadaye Na Mrejesho Mzuri Sana
Kuna ndoa za vodafaster , inafungwa hata katikati ya wiki yaani zoezi ni la nusu saa tu kama ndoa ya mkeka.

Na kuiprocess fasta na masharti yake ni nafuu. Ndoa inafungwa hata na watu 10 tu hapo around no need ya mbwembwe.

Mambo mengi sana ndugu zangu why tuumize kichwa. Shida hawa warembo wetu wanapenda sana attention za mitandaoni ili awaringishie wenzake na kuonyeshana nani zaidi.

Wanaume hatuna mambo mengi sana tunataka ndoa sio harusi.

Sasa kama kwenye hiki kisa, bi dada anataka sherehe ya ndoa jamaa ameshapata ndoa ndo anaishi.
 
Nakazia
 
Aiseeeee..... Shikamooo wanaume jamani.

Maana makwazo hayana budi kujaaaa, ila ole wake yeye akwazayeeee.
 
Ushauri wangu,beba nguo zako nenda kwake km unaenda kumtembelea vile halafu unamaliza huko miezi kadhaa hadi unabeba mimba,ndo inakuwa tiketi.Sometime sisi Wanaume huwa tunakuwa wazito sana kuthubutu hadi tulazimishwe au tubembelezwe.
 
Ushauri wangu,beba nguo zako nenda kwake km unaenda kumtembelea vile halafu unamaliza huko miezi kadhaa hadi unabeba mimba,ndo inakuwa tiketi.Sometime sisi Wanaume huwa tunakuwa wazito sana kuthubutu hadi tulazimishwe au tubembelezwe.
Ndio atakua amesovu tatizo???!! Ameshasema kwasasa tayari ni mjamzito
 
Ndio atakua amesovu tatizo???!! Ameshasema kwasasa tayari ni mjamzito
Basi amefanya kosa kubeba mimba akiwa bado yupo nyumbani kwao, Ilitakiwa ang'ang'ane kubaki kwa huyo jamaa.Sasa Naona usingle mother unamnyemelea.
 
πŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ‘πŸ‘
 
Mahali ikipokelewa tayari kwa desturi wewe umeolewa.
 
Hiyo sio ndoa, ila sheria ina presume hivyo. Hata mkiishi miaka mia kama hakuna ndoa inayotambulika, yaani ya kidini, kiserikali mtu hawezi dai talaka maana hamna ndoa hapo
mkuu naomba kufahamu ,waliooana wakitalakiana kuna mambo ya kugawana mali walizochuma maana hiyo ndoa Sheria inatambua .

Pia kuishi pamoja kwa hiyo miaka 3 inatambulika kama ndoa Ila hamna makaratasi means kuachana haihitaji talaka ,Sasa kugawana mali hapo inakuwaje?
 

Mkuu tofauti iliyopo kati ya wana ndoa na watu walioishi pamoja kwa zaidi ya miaka miwili pamoja kwa kupika na kupakua pasi na ndoa ni kwamba mahusiano ya wanandoa wakishindwana wanaweza kwenda mahakamani kuomba wavunje ndoa (divorce) ama waachane kwa muda wakiendelea kusuruhisha (separation), hawa wa aina ya pili hawana haki hiyo ya kuomba kutalikiana ama kutengana kwa muda sababu in fact kati yao hapakua na ndoa.

Faida yake ni nini sasa hii presumption of marriage? Ni kulinda tu haki za watu waliokua katika uhusiano huo, mfano kama walipata watoto katika hayo mahusiano na wameshindwana itabidi mwanamke aombe mahakama iamuru mwanamme awe analipa gharama za matunzo ya watoto na yeye mwenyewe apewe matunzo lakini pia kama kuna mali walichuma pamoja pindi wakiwa katika huo uhusiano inabidi wazigawane.

In short Yale yote yanayotokea kwa wana ndoa walioona ki halali huku pia yatatokea isipokuwa tu hauwezi kwenda kuomba talaka wala kutengana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…