Amekua mtu wa kununa nuna muda wote

shangwe1

JF-Expert Member
Jan 12, 2017
448
362
Habari zenu wadau,

Jamani mimi ni kijana ambaye nipo kwenye ndoa miaka 2 sasa na tumebahatika kupata mtoto mmoja na huyu mke wangu.

Toka nilivyomuoa tumekua tukiishi kwa amani kabisa lakini sasahivi naona kuna tabia mpya ameianzisha ni tabia ya kununa bila sababu ya msingi, najaribu kumridhisha na kumfurahisha lakini hata hajali.

Hebu nisaidieni wadau atakua na tatizo gani?

Na mimi ni mtu wa kusafirii kila mara kikazi.
 
Ananuna au anadeka?,mtoe out,mkifika huko muulize kwa upendo na mahaba nini tatizo!,pengine kusafiri na kukaa muda mrefu humletea upweke!,ndoa yahitaji uvumilivu mkuu,kila la kheri.
 
Symptoms of postnatal depression

Yaweza kuwa hivyo, so kamuone daktari kwa zaidi asap
 
sasahivi naona kuna tabia mpya ameianzisha ni tabia ya kununa bila sababu ya msingi najaribu kumridhisha na kumfurahisha lakin hata hajali hebu nisaidieni wadau atakua na tatizo gani???
Usiseme bila sababu ya msingi.
Lazima ana sababu ya msingi, ila bado hujaijua.
Wewe unakimbilia kutatua tatizo bila kujua chanzo ni nini..!
Tumia busara zako zaidi kujua sababu ya msingi, usikimbilie kusema hana sababu ya msingi.
Kama hana sababu za msingi, basi unaishi na kichaa bila kujua.
 
Hapo ndipo udhihirishe ni kwa kiasi gani yo mature enough kuwa mume na baba.

Usiseme tu bila sababu za msingi,lazima kuna sababu.
 
Na wewe nuna
Kama ana sababu ya msingi alitakiwa aseme sio kununa
Ukimbembeleza atakuwa akikununia kila siku
 
Kama unavyo sema ni mtu wakusafiri kila wakati hivyo pengine hiyo tabia yako yakusafiri safiri inamkosesha amani yeye na wakati mwingine labda anakabi mpweke sana kuliko muda unaotumia naye pamoja
 
Back
Top Bottom