BABA TUPAC
JF-Expert Member
- Sep 30, 2015
- 1,533
- 3,837
Wakuu,
Mchumba wangu ni mjamzito, ujauzito wake wa una umri wa miezi minne. Yeye yupo Mwanza, mimi nipo Arusha.
Alipoanza kwenda clinic alipewa dawa za kuanza kutumia kwaajili ya madini na madini, ambazo zinakuwa 30 (ambao wameshakuwa wajawazito nadhani wanazifahamu) jina lake limenitoka kidogo.
Sasa leo nimemuuliza hivi zile dawa ulizimaliza? akanijibu kuwa kuna mwenzake wa ofisini alimshauri aache kutumia dawa maana dawa si nzuri, kwahyo alikuwa nusu na nusu aliacha. Niliumia sana kitendo cha yeye kufanya maamuzi yanayohusu mtoto wetu peke yake bila kunishirikisha.
Huyo mwenzake amemshauri kuwa aache dawa na awe anakula samaki au dagaa na mchicha au matembele. Naombeni mnisaidie mambo yafuatayo:
1. Kuna athari zipi mama au mtoto anaweza kuzipata endapo hizo dawa hazitanywewa au kumaliziwa dozi?
2. Kwa amekatisha hiyo dozi karibia mwezi mmoja uliopita, je anaweza kumalizia zile dawa zilizobaki kwasasahivi au kwakuwa alishakatisha dozi inatakiwa aanze upya?
3. Mna lipi na kulishauri zaidi kuhusiana na swala hili?
MWISHO, kina mama msifanye maamuzi yoyote yale kuhusu ujauzito au mtoto peke yako, fanya na mwenzio, msipende sana kusikiliza tu maneno ya saloon na maofisini bila ushauri. Mtoto ni wenu wote, likitokea tatizo lolote wote mnawajibika. Inauma sana, namuonea huruma sana mwanangu na yeye pia mchumba wangu kama kuna athari zozote wanaweza pata
Naombeni sana mnishauri wakuu