amchoma kisu mwenziwe kisa arsanal kula 5

amchoma kisu mwenziwe kisa arsanal kula 5

Babchabi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2012
Posts
1,745
Reaction score
777
Mwanamume raia wa Kenya anayeshabikia klabu ya soka ya Uingereza ya Liverpool amedungwa kisu na mwenzake wa klabu ya Arsenal na kufariki dunia katika eneo la Meru Mashariki mwa Kenya.
Kwa mujibu wa polisi wa eneo hilo wawili hao walianza malumbano baada ya mechi kati ya vilabu hivyo kumalizika hapo Jumamosi.
[h=2][/h]



Wawili hao walikua katika baa moja iliyojaa mashabiki wa timu hizo mbili.
Shabiki wa Arsenal anayefanya kazi ya Boda Boda alijawa na hasira baada ya timu yake kuzomewa na shabiki wa Liverpool na kumfanya kumdunga mwenzake kisu .
Watu waliokua karibu na eneo la tukio hilo walimsaidia mwathiriwa aliyetambuliwa kama Anthony Muteithia na kumpeleka katika hospitali kuu ya Meru ambapo alifariki dunia wakati akipokea matibabu.
Mkuu wa polisi eneo la Meru Tom Odero amesema wanamsaka shabiki huyo wa Arsenal ambaye amekwenda mafichoni.
Hapo Disemba mwaka jana shabiki wa klabu ya Manchester United nchini Kenya kwa jina Jimmy Macharia alijiua baada ya klabu hiyo kuendelea kuorodhesha matokeo mabaya.
Na mnamo mwaka 2012 Suleiman Alfonso Omondi shabiki wa Arsenal alijitia kitanzi baada ya timu hiyo kushindwa kwenye mechi.




[h=2]chanzo bbc/swahili[/h]



 
Although à football is very popular and make à lot of money is just à GAME like any other GAME look what thé players do at thé end of thé GAME they hug each other its not à war Who bewitch you fans? Mario Puzzo thé author of Thé Godfather say "Thé fools die"
 
Back
Top Bottom