Mwanaume mmoja wa nchini Ufaransa amemchinja mkewe kwa kutumia kisu kidogo cha jikoni baada ya kukasirishwa na mkewe ambaye aliamua kuitunza bikira yake na kukataa kumpa unyumba kwa miaka 21 ya ndoa yao kwasababu ya alikuwa hataki kupata watoto.Philippe Cousin mwenye umri wa miaka 53 alimchinja mkewe wa ndoa ya miaka 21 Nicole Cousin mwenye umri wa miaka 47 baada ya Nicole kuendelea kukataa kufanya naye mapenzi kwa kuhofia kupata watoto.
Nicole alikutwa amefariki kwenye nyumba yao katika mji wa Calais kaskazini mwa Ufaransa.
Philippe aliwaambia polisi kuwa mkewe alikataa kufanya naye mapenzi kwa kipindi chote cha ndoa yao akisema kuwa anahofia watoto watakaozaliwa watarithi ugonjwa sugu wa multiple sclerosis (ugonjwa unaosababisha madhara kwenye ubongo na uti wa mgongo) ambao umekua ukimsumbua baba yake Nicole.
Uchunguzi wa maiti ya Nicole ulithibitisha kuwa hadi wakati anafariki Nicole alikuwa kweli ni bikira ingawa alikuwa kwenye ndoa kwa miaka 21.
Siku ya tukio hilo ugomvi ulizuka kati ya Philippe na mkewe ambapo Philippe alichukua kisu na kumwekea mkewe shingoni kabla ya kukikata na kukinyofoa kabisa kichwa chake.
Baada ya tukio hilo Philippe aliwapigia simu polisi na kuwaambia "Samahani kwa kuwasumbua, nimemuua mke wangu".
Phillippe alipandishwa kizimbani jana kwa mauaji hayo aliyoyafanya mwezi aprili mwaka juzi.
Wakili wa Philippe alisema kuwa Philippe alifanya mauaji hayo kutokana na kuchanganyikiwa kimawazo kwa kushindwa kuwa baba.
Philippe ambaye hivi sasa anapatiwa matibabu ya kisaikolojia ndani ya jela huenda akahukumiwa kifungo cha maisha iwapo atapatikana na hatia.
kwa mtazamo wangu nadhani jamaawalikuwa wanaoendana sana maana wangekuwa hawaoendani na si waamninifu to each aza,mwanamke angetoka nje so bikira isingekuwepo n mwanamme angeweza hata kuzaa nje so asingekuwa na msongo kiivyo na stress zingepungua but zoz pple wea zea for each aza
dah!,kweli dunia ina mambo, sasa huyu wife kama aliogopa magonjwa ya kurithi, why akubali ndoa?,kama vp angetumia kinga kuliko kumfanya msela padri..ril astonishment!!!!!!!!!
That's a very patient man! Lazima alimpenda sana mkewe or else asingemvumilia miaka yote hiyo. I'm trying to imagine angekuwa mwanamume wa kibongo ingekuwaje!
mkuu, kama ingekuwa wananyimana, isingefika miaka 21 na wala wasingeuana! hapo ndipo penye shughuli kuelewa!!!!!!!!!!!!!!!!!
ni hivi, kama wangekuwa wananyimana wangekwisha gombana zamani sana nadhani hata miezi sita isingefika wakiwa pamoja!!!!!!!!!!!!!!!!!
inaonekana hawa walikubaliana lakini baada ya muda curiousity ilianza kutafuna akili za mume na ikapelekea mental disorder................ hatimaye murder!!!!!!!!!!!!!!!!
ni suala la kuagalia sana......... wakubwa zetu walikuwa better off kwani hawakuwa na abstinence zenye longer terms........... ndoa zilifungwa na vijana sio izi watu wanaoana wakiwa kwenye 30s !!!!!!!!!! na ukizingatia kuwa walipevuka kwenye late teens!!!!!!!!!!! majaribu natupu!!!!!!!!!!