Ambayo ulikuwa huyajui kuhusu zitto

Ambayo ulikuwa huyajui kuhusu zitto

Joined
Apr 12, 2013
Posts
15
Reaction score
5
[h=5]INAUMA SANA,japo wanasema ukiwa safarini haupaswi kuwaulizia njia unaokwenda nao bali wanaotoka huko uendako bt sometimes napata mashaka na majibu nitayopewa.

mwaka 2010, sebastian kasinge aliyeteuliwa kugombea ubunge jimbo la mpanda mashariki, alikwama kuwania nafasi hiyo. Kisa?! Zitto.ilikuwa hivi, kasinge alikwama kupata barua ya utambulisho kutoka kwa viongozi wake wa wilaya ya mpanda kuwa ni mgombea. Akaenda makao makuu ya chadema jijini dar es salaam. Akakutana na dk. Slaa, katibu mkuu wa chama chao, akampa barua ya uteuzi.lakini zitto kwa kutumia kofia yake ya unaibu katibu mkuu tena akiwa nje ya ofisi na bila kushirikiana na wenzake wa makao makuu, alimwandikia msimamizi wa uchaguzi wilaya ya mpanda kumjulisha chadema kutoweka mgombea jimbo la mpanda mashariki. Msimamizi wa uchaguzi mara baada ya kupata barua ya zitto alimwondoa kasinge kwenye kinyang'anyiro cha ubunge na kumtangaza mgombea wa ccm, mizengo kayanza peter pinda kuwa amepita bila kupingwamichael makenji aliyekuwa mgombea wa ubunge wa chadema jimbo la musoma vijijini, alijiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho dakika za mwisho. Nimrod mkono wa ccm alipita bila kupingwa. Hii ni baada ya zitto kumshawishi mgombea wa chama chake kujitoa. Taarifa zinazomkhusu makenji zinasema kabla ya mgombea huyo kujiondoa kwenye kinyang'anyiro, naibu katibu mkuu wake alifanya mazungumzo ya kina na mkono.katika kuthibitisha hilo, makenji alikabidhi kwa viongozi wake wa chama ujumbe mfupi wa sms ulioonekana umetoka kwa zitto kwenda kwake ukilenga kumshawishi kujitoa.miongoni mwa yale yaliyotajwa na zitto kwenye ujumbe huo ni pamoja na kwamba mkono yupo tayari kuongeza fedha iwapo yeye makenji atakubali kujiondoa kwenye mbio za kuwania ubunge.josephat isango, aliyejitosa kwenye mbio za ubunge jimbioni singida kupambana na mohamed dewji aliwekewa pingamizi na wazael nakamia, mwenyekiti wa chama chake, chadema wilaya ya singida mjini. Katika pingamizi lake, nakamia anasema isango hakupitishwa na chama chake kugombea nafasi hiyo. Alipoulizwa na mkurugenzi wa sheria wa chama hicho, tundu lissu kilichosababisha kuwekewa pingamizi kwa ndugu isango, nakamia alisema ..."ni maelekezo ya naibu katibu mkuu..."zilitokea vuta nikuvute kadhaa ambapo mwishowe dk. Slaa ambaye alikuwa amelazwa hospitali ya taifa ya muhimbili kwa matibabu alimwandikia msimamizi wa uchaguzi barua nyingine ya kuthibitisha uteuzi wa isango.rais kikwete alipofika singida kumnadi mgombea wa ccm singida alimtangaza dewji kuwa amepita bila kupingwa, siku chache baadae nec ikamtangaza isango kama mgombea.tamthilia hii ya isango, zitto, dewji, nakamia na lissu imeelezwa mara nyingi na na lissu mwenyewe kwenye vikao vya cc mbele ya zitto wenyewe. Zitto hakuwahi kukana. Nakamia tayari amevulia uongozi.mgogoro wa madiwani arusha haukumalizika bila ya kumhusisha zitto. Kamati iliyoundwa na chama chake kutfuta suluhu ya mgogoro huo iligundua mkono wa zitto katika suala hilo. Mgogoro ule uliisha kwa kufukuzwa madiwani watano.naibu katibu mkuu alishiriki kwa kiasi kikubwa katika mgogoro huo kwa kushiriki kuwashawishi madiwani kukiasi chama, ni sehemu ya mkakati wake wa kupambana na lema na wanasiasa wenzake ndani ya chama chake wanaoonekana kumpiku kwa umaarufu.uchaguzi mdogo ulipofanyika zitto hakushiriki hata mkutano mmoja wa kampeni,hkwenda arusha siku ya maombolezo baada ya vifo vya wafuasi wanne wa chadema.mengi zaidi soma mawio, toleo namba 0070 alhamis november 21-27, 2013 uk10-11[/h]
 
siku zote tulikuwa tunakata matawi na kuacha shina likiendelea kumwagiwa maji na jirani mtani ila leo shina limekatwa na kung'olewa mizizi yote,jirani hajalala,anapiga kelele usiku kucha.

kuna mpango mkakati nimeuweka kwenye uzi wangu moda wameutoa ila yote niliyosem mtayaona in a wide creen
 
Back
Top Bottom