Amateur Government?

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
16,102
25,974
Kati ya mambo yanayonishangaza awamu hii ni teuzi za Mh Magufuli.
Teuzi zimejikita katika vyo kuwaibua maprofesa na madaktari wa ngazi za PhD katika kuongoza Idara nyingi.

Kinachonishangaza si teuzi zenyewe lakini jinsi ambavyo wanaoteuliwa katika nafasi za utendaji, si tu wametumikia nje ya idara husika lakini hawana uzoefu unaohitajika kwa weledi.

Wanasiasa ni rahisi, wanapiga siasa popote pale wanapowekwa.

Serikali ni watendaji wake, na watendaji wamesukwa sukwa hadi kufikia ngazi za juu kwa sababu ya uelewa wa utendaji na vile vile weledi na uzoefu.
Mtu akifika ngazi ya Ukurugenzi mawizarani ujue amewiva kufikia ukatibu mkuu, na hapo ana uzoefu wa si chini ya miaka 20 sehemu yake ya kazi.

Utendaji wa mfanyakazi wa serikali huishia ukatibu mkuu, ngazi ambayo ni ya juu kanisa.
Katibu Mkuu anatakiwa kuwa na uzoefu usiotia shaka katika eneo lake la kazi, na ndiye accounting officer wa mwisho katika serikali, katika wizara husika.

Siyo siri, hili la kuteuliwa Profesa Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wizara ya Maji na Umwagiliaji, imenishangaza.

Alikuwa anafanya research na kuendesha lectures chuo kikuu, an academic role.
Leo ni Katibu Mkuu a technoctratic and beureucrat role.
Na wako wengi wa aina hiyo.

Anyway yote yanawezekana, ngoja niendelee kushangaa shangaa miye.
 
Hawajifunzi tu ,mmoja wa walioharibu elimu ya Tanzania anaitwa Sifuni Mchome kwa kushirikiana na Mulugo , hawa wawili walianzisha Div 5
 
Back
Top Bottom