Amani Thani anaelezea historia ya Abdallah Kassim Hanga

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,791
31,803
  1. AMAN THANI ANAELEZA HISTORIA YA ABDALLAH KASSIM HANGA SEHEMU YA KWANZA

    Utangulizi

    Marehemu Mzee Aman Thani hakuingia kaburini na elimu yake. Kaacha nyuma elimu katika historia ya siasa za Zanzibar kama hidaya kwa vizazi vijavyo. Kwanza kwa kuandika na kitabu chake mashuhuri ni ‘’Ukweli ni Huu.’’ Pili, kwa kutoa mihadhara mingi. Katika moja ya mihadhara yake inayosisimua, kuelimisha na kufikirisha ni huu mhadhara aliotoa wa maisha ya kinara wa mapinduzi ya Zanzibar, Abdallah Kassim Hanga. Hanga ni katika historia ya kusikitisha sana katika Mapinduzi ya Zanzibar kiasi kwamba hata wanamapinduzi wenzake kwa nusu karne walikuwa kimya hakuna aliyependa kumtaja. Hata katika kusheherekea miaka 50 ya mapinduzi, walipotoa medali za waliofanisha mapinduzi yale, jina la Abdallah Kassim Hanga, halikuwako. Naona fahari kuwakilisha sehemu ya kwanza ya mhadhara wa marehemu Aman Thani mmoja wa wazalendo waliopigania uhuru wa Zanzibar. Mhadhara huu aliufanya nyumbani kwake Dubai, Rashidiya.

  2. Mohamed Said: AMAN THANI ANAELEZA HISTORIA YA ABDALLAH KASSIM HANGA SEHEMU YA KWANZA

    Posted 2 hours ago by Mohamed Said
    Labels: historia
Loading

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom