nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,803
Na Daniel Mjema,Mwananchi
Posted Jumatano,Aprili10 2013 saa 15:1 PM
Chadema inadai wapandaji wa mbegu ya udini ni CCM
Moshi. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema iwapo amani itatoweka kutokana na vurugu za kidini, watawashtaki viongozi wa CCM Mahakama ya Kimataifa ya The Heague.
Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na Mwenyekiti wa Chadema Manispaa ya Moshi, Jaffar Michael wakati akimkaribisha Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo kuhutubia mkutano wa hadhara.
Michael ambaye pia ni Meya wa Manispaa ya Moshi, alisema baadhi ya viongozi wa Serikali ya CCM ndiyo kiini cha mbegu za chuki za kidini, walipoituhumu Chadema kuwa ni chama cha kidini.
Nataka niwaambie leo, amani ya Tanzania ikivurugika tunawapeleka viongozi wote wa Serikali ya CCM The Heague, wao ndiyo chanzo cha chuki hizi za udini ambazo zinaligawanya taifa, alisema Michael.