Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kimepokea majeruhi 21 wanaodaiwa kujeruhiwa na askari wa Jeshi la Polisi katika tukio la Aprili 24, 2025, wakati wakielekea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia kesi ya mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, Amani Golugwa amesema majeruhi hao walikamatwa, kupigwa na kupelekwa katika pori la Mabwepande, huku wengi wao wakiripotiwa kuwa katika hali mbaya.
"Tukio la jana mpaka kufika usiku tulipokea taarifa ya majeruhi 21 ambao walikamatwa na polisi, wakapigwa sehemu mbalimbali za miili yao, wakapakiwa kwenye magari ya polisi na kupelekwa Mabwepande," amesema Golugwa leo Ijumaa Aprili 25, 2025, katika mkutano na waandishi wa habari unaofanyika Makao Makuu ya Chadema, Mikocheni, Dar es Salaam.
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limethibitisha kuwakamata na baadaye kuwaachia kwa dhamana viongozi na wafuasi watano wa Chadema waliokuwa katika eneo la Mahakama ya Kisutu, likisema kuwa walihusishwa na mkusanyiko usio rasmi katika kipindi cha kesi ya Lissu.
Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa usiku wa Aprili 24, Polisi imeeleza kuwa: “Kazi ya kuzuia vitendo vya kihalifu inaendelea kwani hilo ndilo jukumu kubwa la msingi la Jeshi la Polisi.”