Ama kweli wanasiasa wana ndimi mbili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ama kweli wanasiasa wana ndimi mbili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bbukhu, Oct 10, 2012.

 1. b

  bbukhu Member

  #1
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MAKALA

  AMA KWELI WANASIASA WANA NDIMI MBILI

  Mwishoni mwa mwezi Agosti, waziri wa Afrika mashariki bwana Samwel Sitta aliibuka na kudai kuwa chama cha demokrasia na maendeleo hakina viongozi wa kutosha wa kufanya kazi ya serikali zaidi ya Dr Slaa. Kwa hiyo muda wake wa kutawala nchi bado!
  Sitta aliliyasema hayo wilayani karagwe Mkoani kagera katika ziara ya yake ya kutembelea ofisi ya ccm wilayani karagwe. Namnukuu. " Hawa jamaa hawana hazina ya viongozi wa kama tuliyonayo ccm, ambapo tunaweza kuwasimamisha wagombea 20 wenye sifa zinazofanana tofauti na wao wanaye Dr Slaa tu ambaye inasemekana aliukimbia upadri" Kwa kauli hiyo Sitta anaamini kuwa ndani ya chadema kuna mtu moja tu mwenye sifa ya urais ambaye ni Dr. Slaa na ndani ya chama chake cha ccm kuna watu 20 wenye sifa za urais!

  Kauli hiyo ya Sitta imenikumbusha kauli aliyoitoa waziri mkuu mstaafu ndugu Fredrick Sumaye katika moja ya kampeni za uchaguzi wa 2010 wilayani Hanang' Mkoani Manyara. Katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika kaitka kata mpya ya Endasiwold Wilayani Hanang' huko Manyara, Sumaye aliwahi kusema kuwa chadema haina umbo la kuongoza nchi, Dr. Slaa ameningi'nia kwenye mti usio na mizizi na akasema pia kuwa Dr. Slaa hata akipewa urais hataweza kuwapata watakaomsaidia!

  Nimekumbuka kauli hiyo ya Sumaye kwa kuwa inashabihiana na ya Sitta. Kauli za viongozi hao wa ccm zinadhihirisha kuwa wanasiasa ni watu wenye ndimi mbili yaani vigeugeu. Leo hii wakitumia ulimi moja kusema jambo fulani kesho watatumia ulimi mwingine kusema jambo lingine lenye utata. Watu hao ni hatari sana katika jamii yetu. Ni watu ambao hawako tayari kufanya kazi kwa maslahi ya wapigakura waowanaoishi pembezoni mwa nchi.

  Kauli hizo zilizowahi kutolewa na Sitta na Sumaye kwa wakati tofauti hazina ukweli wowote bali zinalenga kuwahadaa watanzania ambao wamezongwa na umaskini, dhuluma na unyanyasaji. Watu wenye sifa za urais wanaweza kupatikana katika chama chochote cha siasa na wanaweza kupatikana hata miongoni mwa watu wasio na chama chochote cha siasa kwani urais hausomewi. Hata mtu mwenye elimu ya kidato cha sita anaweza kuwa rais wa nchi.

  Mheshimiwa Sitta anadhani kuwa nchini Tanzania wasomi na watu wenye sifa za urais wapo ndani ya ccm peke yake! Najua hata ccm walikuwa na watu safi wenye sifa za urais lakini watu hao wametupwa nnje ya mfumo wa kisiasa kwa kuwa msimamo wao hauendani na maslahi ya wazee wa ccm na ambao ndio wenye chama kwani ccm inahitaji watu vigeugeu na wanaoweza kulinda ufisadi ndani ya chama

  Kiongozi kama Samwel Sitta ambaye ni kigeugeu au mwenye ndimi mbili asingestahili hata kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa kijiji maana hafai kuwa kiongozi. Kiongozi anapaswa kuwa mtu mwenye msimamo usio tetereka. Samweli Sitta kuna wakati alinusurika kuvuliwa uanachama kwa madai kuwa alikuwa anakiuka maadili ya chama! Ccm haikupendezwa na hatua ya Sitta kuruhusu wabunge kuibua na kujadili kashfa za ufisadi bungeni katika kampuni ya Richmond na kuundwa kwa kamati teule iliyochunguza kampuni ya Richmond. Baadaye Sitta akajirudi na rais akampa uwaziri sasa hivi anakazi ya kutetea chama chake.

  Tunakumbuka wakati akiwa spika, Sitta alitumia ubabe kuwazuia wabunge kujadili baadhi ya masuala mazito yaliyokuwa yanadaiwa na serikali kuwa ni maslahi ya taifa! Tunakumbuka mwaka 2008 moto ulipowaka bungeni kutokana na sakata la Richmond hatimaye Sitta akakubali kwa shingo upande uundwaji wa kamati teule ya bunge kuchunguza kampuni ya Richmond. Kamati hiyo iliongozwa na Harisson Mwakyembe lakini hata hivyo kamati hiyo ikaficha baadhi ya mambo kwa madai ya kulinda maslahi ya taifa. Wabunge wakiwamo wa ccm wakajadili kwa nguvu ripoti ya kamati teule iliyochunguza Richmond lakini cha kushangaza ni kwamba leo hii kila kitu kimeshafunikwa ni kana kwamba hakukuwa na ufisadi wowote wakati ufisadi umeota mizizi kwenye kila sekta. Leo hii Sitta anaamini kuwa wenye sifa za urais wapo ndani ya ccm peke yake! Chama kinacholea na kulinda ufisadi.

  Je, kwa mantiki hiyo Samwel Sitta na wale wabunge wenzake wote wa ccm waliokuwa wanatoa machozi bungeni kujadili mambo ya Richmond na EPA, leo hii wamegeuka tena na kuitetea ccm na serikali yake wana sifa zipi za urais? Aidha tunakumbuka mwaka 2009, wakati Sitta akiwa spika wa bunge alidai kuwa tuhuma za ufisadi na/ au wizi mkubwa wa fedha za umma unaoyahusu makampuni ya MEREMETA ltd, TANGOLD ltd na DEEP GREEN FINANCE co.ltd haziwezi kuzungumzwa ndani ya bunge kwa sababu tuhuma hizo zinahusu mambo ya jeshi au usalama wa taifa! Kauli hiyo pia ikaungwa mkono na waziri mkuu, Mizengo Pinda. Huyu ndiye Samwel Sitta ambaye leo anadai kuwa ccm ina watu zaidi ya 20 wenye sifa za urais!

  Watanzania tunapaswa kutambua kuwa wanasiasa ambao wanatetea chama kinacholinda ufisadi hawafai kuwa viongozi kwani wanahatarisha amani na usalama wa nchi. Kiongozi anapaswa kuwa mwadilifu, mwazi,anapaswa kusilikiliza maoni ya watu, asiyependa ufisadi na mwenye kujali shida za watu.


  Na Barnaba Bukhu
  0784195782
  Barua pepe: bbukhu@gmail.com
   
 2. Adoe

  Adoe JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Asante lakini hapo kwenye red, mmhh?

   
 3. M

  Mr jokes and serious Member

  #3
  Oct 10, 2012
  Joined: Oct 4, 2012
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa nijinc gani wanavyo wafanya watanzania wajinga waclete sababu zisizo za msingi wabadilike kutokana na wakati,hawandio leo hii unaweza kuwa ckia chagua ccm chama kilicho leta uhuru wanavyo wadanganya vijijini uko,uhuru alafu m2 ana lala njaa wapi nawapi hapo,awa wa2 wakuwaangalia sana hawa,mimi ninawaelewa m4c wanavyo enda vijijini najua watawasaidia watanzania wenzetu wanaodanganywa na khanga na chakula pesa,na kofia.watu wanaumia jamani vijijini uko nyie acheni 2 hali mbaya jamani.
   
 4. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  CCM inaviongozi wanafiki akina sita,sumaye,mukama,nape,makamba,mwigulu,.......duuuh kumbe wote wanafiki!!
   
 5. t

  thatha JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Kazi ya bunge ni kuisimamia Serikali na siyo kuipinga Serikali. Sijaona kosa la Sitta, wakati akiwa Spika alikuwa anafanya kazi ya kusimamia serikali ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Kufanya hivyo hakumaanishi lazima kuipinga serikali kwa kila jambo. Jmabo la msingi tunalotakiwa kulitambua ni kwamba Kusimamia Serikali ni tofauti na kuipinga Serikali.

  Kwa kifupi tu ni kwamba kwa siasa zetu changa za kiafrika, BUNGE LINASIMAMIA SERIKALI NA SIYO KUIPINGA SERIKALI na kutokana na siasa za maji taka za kiafrika , WANASIASA NDO WAPO KUIPINGA SERIKALI JAPO HAWAJUI WANALOLI
  TENDA NI TOFAUTI NA MADHUMUNI HASA YA MFUMO WA VYAMA VINGI.
   
 6. S

  Starn JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 400
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Unajua neno SIASA lilitokea wapi?- Lilianzia kwenye neno SIHASA maana yake ni kwamba wanasihasa hawamaanishi kile wanachosema siku zote.
   
 7. D

  DR. RICHARD Senior Member

  #7
  Oct 10, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 127
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tatizo la hao watu hata kusoma vitabu vya historia ya Africa wamestaafu wanawaza kuiba 2,

  Kwame Nkhruma, mwaka 1958 anasema "WAPE WATU KUONGOZA ILI WAJIFUNZE KUONGOZA" hapa ni pale ambapo wazungu walikuja na hoja kama hiyo ya kwamba Ghana haiwezi kujitawala kwa sababu haina watu wenye uzoefu/ sifa, kwani Tanu walipata wapi viongozi?
   
Loading...