Ama kweli mapenzi yana wenyewe!

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
Hivi ilishawahi kukutana na ile situation umekutana na mwanamke barabarani, kila unapojaribu kuzungumza naye, yeye haoneshi attention yoyote ya kuzungumza ama kuvutiwa na wewe! imani yangu watu wa namna hiyo ni wachache kukuta anapewa details sahihi na mwanamke huyo! just imagine unamwongelesha ilhali yeye amenuna na anaendelea na mawazo ya mishe zake kama kawaida!

Siku ya leo nimeshuhudia kisa cha tofauti kidogo!

Wakati wa asubuhi nikiwa naelekea kwenye shughuli za hapa na pale ili kupata pesa kwa ajili ya mahitaji ya familia na mafuta nilikuwa sambamba na mwanadada ambaye alikuwa mbele yangu. Ghafla bodaboda mmoja tokea nyuma yangu akasogea mpaka mahali mwanadada alipo kisha kumuomba yule mwanadada apande ili ampe lift! mwanadada yule akakataa japo alikuwa akitabasamu!

Bodaboda yule ndo kujipa imani kuwa hakuna mkate mgumu mbele ya chai kwamba mwanadada yule hataki kujionesha kuwa yeye ni maharage ya mbeya ya maji jagi moja.

Waliendelea kujibizana story za hapa na pale huku wakitabasamu! Muda huo mwanadada akiwa anatembea kwa miguu na huyu bodaboda akiwa analazimisha pikipiki yake kwenda taratibu mithili ya mwendo wa kobe mchafu! Wakati wametembea umbali mrefu kidogo, bodaboda kajikuta akiteleza na kiangukia kwenye mtaro ulio pembezoni kufuata ile barabara! tena mtaro wenye matope mazito kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Yule mwanadada, alipoteza sura yake ya kutabasamu! na kuweka sura ya kazi! alitazama mbele aendako! hakudiriki kutazama pembezoni kuona kama mwangukaji kaangukia kiuno ama dushe! akatembea mbele kwa mwendo wa jeshi huku akiziseti nywele zake zilizokuwa zikishikwa na yule bodaboda aliyekosa kazi.

Ndipo nilipofika eneo la tukio, pamoja na watu wengine ili kuiopoa pikipiki yake! Hajaumia sana lakini.

Dada wa watu aliishilia na kutokomea kusikojulikana.

Ama kweli, Mapenzi yana wenyewe! Hakuambulia hata namba ya simu!!
 
Wadada kwenye kutoa msaada wanajifanyaga hawawez,mnakwama pamoja mpo kwenye gari lakini hashuki unatafuta wa kukusukuma yupo ndani ya gari anachezea smart tu.

Dawa yao kama ni mwanamke wako baada ya kutoka hapo inatakiwa ukampelekee moto wa hatari kulipiza hicho alichokifanya
 
Huwezi kuwa mpenz wa kilamtu na si kila mwanamke barabarani hana mpenz.Ivo ni kawaida
Kwani mkuu, Kwa dunia ya sasa kuna mwanamke ambaye hayuko kwenye mahusiano kweli!?

Wanawake wa sasa, akisalitiwa leo, kesho asubuhi anatafuta pa kuegemea!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom