Miaka 4 nmeishi kama shetani nisie na mbele wala nyuma , hiyo ni baada ya uko nyuma kuchezea hela . Nilizani sifa walizokuwa wananipa walimaanisha nikajiona napendwa kila kona napopita yeyote akiniomba buku Nampa buku mbili, wa elfu tano Nampa bila kujiuliza mara mbili , kumbe ilikuwa inapendwa pesa tu sikujua ilo , nilivoishiwa sikumuona yeyote kati yao sio ndugu , sio rafiki, walaa wale mademu waliokuwa kutwa kuniita beb... Kwenye simu yangu walibakia watu wawili tu waliobaki kunitafuta na kunijulia hali , Mama yangu na mke wangu pekee ndo walibakia kuwa wafariji wangu.... Leo Mambo yamerudi kuwa sawa baada ya msoto mkali , kiukweli nmejifunza vitu vingi sana ... Pesa yangu kuja mtu kuila kizembe sio rahisi aisee , pesa yangu saiv inaenda kwenye vitu muhimu pekee ....