Nauliza,
•Hivi zile za push-ups jukwaani ziliishia wapi? Bado zinaendelea? Tutumie nguvu hizo kulegeza vyuma vilivyokaza.
View attachment 977550
View attachment 977551
•Milioni 50 kila kijiji ziko wapi? Zimehamia miundombinu? Kupanga ni kuchagua.
View attachment 977548
•Wakulima wasipangiwe bei, je, wanapangiwa au hawapangiwi? Korosho hoyeeee?
Nadhani sasa hivi mbuzi wanakunywa champagne badala ya bia.
View attachment 977559
•Watumishi wataboreshewa maslahi, nadhani wanasherekea, au siyo?
Wakishindwa kupanda madaraja wapande ndege!
View attachment 977566
View attachment 977564
•Mahakama ya mafisadi imewahukum kina nani? Kina Mbowe? Akram?
Vipi waliouza nyumba za NHC? Escrow? Richmond? Iptl?
•Mikopo vyuo vikuu,
neno lenyewe mkopo? Wanachuo, hali ikoje huko?
•Tumbua, teua, zimeleta tija?
•Kauli yetu ya Hapa Kazi Tu, bado inavuma majukwaani? Vipi serikali ya viwanda?
•Wafanyabiashara sasa nadhani mna mazingira mazuri ya kufanyia biashara, mtatuangusha 2020? Wamachinga hoyee!
Mmeshapata kipande?
•Elimu bure safiii, na nyie dada zetu, kwanini mnakuwa wazazi kabla ya F4? Msitulaumu.
•Huduma za afya vijijini safi, lakini na nyie wananchi
kwanini mnakataa kukata bima CHIF kwa sh.15,000/=?
Tunawatakia sikukuu njema.
View attachment 977570