Ama kweli "IVUMAYO HAIDUMU"

Ama kweli "IVUMAYO HAIDUMU"

Trust None

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2018
Posts
1,260
Reaction score
4,421
Nauliza,
•Hivi zile za push-ups jukwaani ziliishia wapi? Bado zinaendelea? Tutumie nguvu hizo kulegeza vyuma vilivyokaza.
IMG_0159.jpg

Push up.jpg

•Milioni 50 kila kijiji ziko wapi? Zimehamia miundombinu? Kupanga ni kuchagua.
48413151_582961848878160_5937223800553734144_n.jpg

•Wakulima wasipangiwe bei, je, wanapangiwa au hawapangiwi? Korosho hoyeeee? Nadhani sasa hivi mbuzi wanakunywa champagne badala ya bia.
aes.jpg


•Watumishi wataboreshewa maslahi, nadhani wanasherekea, au siyo? Wakishindwa kupanda madaraja wapande ndege!
1e42ef80d717acd97c5277a7af038769.JPG

Dreamliner.jpg

•Mahakama ya mafisadi imewahukum kina nani? Kina Mbowe? Akram? Vipi waliouza nyumba za NHC? Escrow? Richmond? Iptl?

Mikopo vyuo vikuu, neno lenyewe mkopo? Wanachuo, hali ikoje huko?

Tumbua, teua, zimeleta tija?

•Kauli yetu ya Hapa Kazi Tu, bado inavuma majukwaani? Vipi serikali ya viwanda?

•Wafanyabiashara sasa nadhani mna mazingira mazuri ya kufanyia biashara, mtatuangusha 2020? Wamachinga hoyee! Mmeshapata kipande?

Elimu bure safiii, na nyie dada zetu, kwanini mnakuwa wazazi kabla ya F4? Msitulaumu.

•Huduma za afya vijijini safi, lakini na nyie wananchi kwanini mnakataa kukata bima CHIF kwa sh.15,000/=?

Tunawatakia sikukuu njema.
48419340_2494451403915494_9031823406055555072_n.jpg
 
Ha ha push up kama ameacha kusema serikali ya viwanda amebakiza kauli za Mimi sitikisiki sijaribiwi sitishwi hamtalipwa fidia korosho nitanunua Mimi nitachonga Tanzanite hapa gesi inauzwa yote ulaya TRA hamkusanyi mapato ujuwe Magufuli kashindwa kuendesha nchi
 
Ha ha push up kama ameacha kusema serikali ya viwanda amebakiza kauli za Mimi sitikisiki sijaribiwi sitishwi hamtalipwa fidia korosho nitanunua Mimi nitachonga Tanzanite hapa gesi inauzwa yote ulaya TRA hamkusanyi mapato ujuwe Magufuli kashindwa kuendesha nchi
Bado miaka 7 mpaka mfike ZIMBABWE.
 
Inavyopiga push ups huwezi hisi kama ni binadamu kama mirobot!
 
Back
Top Bottom