am tired...

ndusyepo

Senior Member
Joined
Jul 2, 2013
Posts
167
Reaction score
50
hivi wana jf naomba mnifahamishe ..hivi unapoamua kumwoa mwanamke yeyote tk familia yeyote ,pale unakuwa umemwoa huyo mwanamke au umefunga ndoa na ukoo wake mzima?
 
Mkuu Ndusyepo jina lako tu linaonyesha umechoka unahitaji kupumzika, naona familia ya wife imeamua kuhamia kwako, ki ukweli unakua umeoa mke na wale wengine wanakuwa ni ndugu zako tu, so kama wameamua kuja kwako ni kwa sababu hawako vizuri wanaona kwako ndio pa kuponea, na pia kuna baadhi ya makabila hii ni tabia ya kawaida kabisa.
 
Hakuna kitu sipendi kama kiringi nyumbani kwangu........njoo salimia ondoka......
 
Inategemea kama ulijifaragua ndio madhara yake ,mwanamke mwenye akili atailinda familia na ndoa yake ,atamwacha baba na mama yake ambatane na mumewe hii ni biblia takatifu .sidhani kwa imani yangu hujaoa hiyo familia yake kama ni kuwapa ni moyo wako tu sio lazima.
 
ndusyepo

Mbona wao walikuamini na kukukabidhi mwanao, iweje leo unaanza kuwatenga?

Tubhule kanunu nkamu...fiki hifi fikukutamya?
 
Last edited by a moderator:
duuh pole ndugu ila usiumie roho wakati duniani unaishi mara moja tuu. Ongea na wife wako kwa nia nzuri tuu na kwa lugha nzuri isiwe ya kumsimanga. Kama wamekuja hapo kuhitaji msaada nawe unaona umelemewa ni vyema mkakaa kikao myaongee kwamba uwasaidie wakiwa kwao na si hapo kwako ili uwe na amani na nyumba yako ni ngumu ila ukweli utakuweka huru, mjini hapa watu wanaishi kwa budget. Kama wamekuja tuu hawahitaji uwezo kivileee wasepe na wasikuwekee kiwingu maana ndugu ukikaa nao sana wanakwaza. Kuna ndugu anajisikia kuja kukaa kwa shemeji kisa anakimbia kazi kwao au kubanwa so anataka uhuru hapo na wanakuja kibao hata siku unakuja na wageni wako unakuta wamejaa sebleni na hata hawakupishi wewe ndo uanze kuhangaika na wageni wako wakati uko home kwako, hapo ni kuwatawanya tuu kila mtu arudi kwao ubaki na wife.
Kama ndo wamefata msaada na kweli wewe ndo unawasaidia huna budi kuwaambia unahitaji likizo wakapumzoike kwao na baada ya hapo misaada itawafata hukohuko kuepusha makwazo. Kama ni shule wasome za karibu na kwao au boarding pia ndugu wengine kwenye familia nao wachangie isiwe wewe tuu waambie kuna kuchoka.
 
hivi wana jf naomba mnifahamishe ..hivi unapoamua kumwoa mwanamke yeyote tk familia yeyote ,pale unakuwa umemwoa huyo mwanamke au umefunga ndoa na ukoo wake mzima?

kwani wewe ulitoa mahari ya watu wangapi?
 

yani dawa yao timua wote
nimeoa/olewa na mmoja bana
waje wasalimie na kusepa na sio kila siku wageni!!

 
wanandugu wengi ndio wako hivyo.....

hadi kuendelea inakuwa ngumu,maisha yenyewe
magum,watu wanakuja kujazana home loh
 
Ndio muwe mnaoa born hiahia ila sisi wa kijijini bwana ,mmoja akibahatika kuolewa mjini hapana chezea ukoo mzina lazima uhamie kwa bwashee kula maraha ya darisalama
 
Baba mkwe na mama mkwe nitawavumilia lakini kaka na dada sijui mjomba na shangazi kwakweli nitawatoa baruti mbaya.
 
Kha, hii post imechangiwa na watoto wakareeee..kuanzia Preta, Mkunde original, Double k, Heaven on earth, Toria, dismyndert.....Nabhata ushungu wallaahhhh!!
 
hivi wana jf naomba mnifahamishe ..hivi unapoamua kumwoa mwanamke yeyote tk familia yeyote ,pale unakuwa umemwoa huyo mwanamke au umefunga ndoa na ukoo wake mzima?
Na hapo ndo mnapoambiwa angalieni makabila mnakoowa..... tatizo lenu mnadhani huo ni uzamani...
1. Owa mndengereko uagwe kwenda ngomani kila kukicha..... au anapiga halafu mdundiko unakatiza... keshoooo hiyooo ndo atarudi...
2. Owa mndengereko, akujazie dada zake walioachika kwa sababu ya ngoma hupo kwako...
3. Awa mchaga na upate mali na baada ya hapo jiandae kufa...
4. Owa mara halafu ujifanye mmbabe, uone kaka zake watakavyokuja na mapanga...
5. etc... etc...
 
Unadhani wanapokuja mkeo/mumeo anakuwa hajui..??? We mtoe baru halafu uone kitakachofuata toka kwa mkeo/mumeo


Sijui kwako mkuu, lakini kwangu mimi kama baba mwenye nyumba kauli yangu huwa haiulizwi kwanini. Sijasema wasije kabisa lakini kama anakuja likizo katoka shuleni hapo sawa lakini ile ya kuweka kambi kabisa yupo yupo tu analala na kuamka huku hana uelekeo kwakweli hapo nitaonekana mmbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…