MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
MBUNGE wa Nkasi, Ally Keissy (CCM) amewataka wabunge wa upinzani waache kusakama uteuzi wa Profesa Sospeter Muhongo kuwa Waziri wa Nishati na Madini kwani si fisadi.
Kessy aliyasema hao kufuatia Msemaji wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni kwa wizara hiyo, John Mnyika kusema ''Mweshimiwa Rais Magufuli bila kujali nini bunge lilikwishaazimia katika kikao ambacho na yeye alikuwa sehemu ya azimio hilo lakini bado akamteuwa Prof. Muhongo kuendelea kuiongoza wizara hii, Kambi rasmi ya Upinzani inaliona jambo hili kama ni dharau sana kwa bunge na fedheha binafsi kwa Rais Magufuli''.
Kessy alimpongeza Rais John Magufuli kwa kumteua Muhongo kwani hajakosea na anajua ni mchapakazi. “Watu wanalalamikia uteuzi wa Profesa Muhongo wakati hakuhusika na Escrow. Katika Bunge la Tisa aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa alijiuzulu kwa kashfa ya Richmond,” alisema Keissy.
Aliwashangaa CHADEMA kumtembeza Edward Lowassa kote nchini wakimuombea kura wakati alijiuzulu Uwaziri Mkuu akituhumiwa kwa ufisadi. Akichangia makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka 2016/17 bungeni jana, Keissy alisema Profesa Muhongo hahusiki na sakata la akaunti ya Tegeta Escrow.
Alisema, “Mlimchukua Lowassa ambaye alijiuzulu kwa kashfa ya Richmond mkatembea naye nchi nzima kumuombea kura awe rais. Leo angekuwa rais sijui ingekuwaje. Mmekuwa kama kuku wa kizungu, mnasahau haraka.” Lowassa alikuwa mgombea urais kupitia Chadema kwa mwavuli wa Ukawa katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Alihama CCM baada ya kukosa uteuzi ambao ulimuibua Dk Magufuli kuwa mgombea. “Rais Magufuli hana siasa, anachagua wachapakazi. Halafu mnasema Muhongo kahusika na Escrow. Waliohusika na Escrow wametajwa, na wala hakuchukua kiroba cha hela. “Huyu ni mteule wa Serikali ya CCM wala hatabanduka pale.
Mmejipiga huko nyuma, sasa mtacheka wenyewe. Mmeboronga na mtapungua siku hadi siku, kaeni chonjo,” alisema Keissy. Baada ya mbunge huyo kumaliza kuchangia, Spika Job Ndugai aliyekuwa akiongoza kikao cha jana asubuhi, alisema, “mlichokoza wenyewe.”
Chanzo: Habarileo