Ally Kessy: Bunge linapoteza 40m kila siku kutokana na wabunge hewa

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787


Mbunge wa jimbo la Nkasi Kaskazini Ally Kessy amesema kuwa kwa siku bunge linapoteza milioni 40 kutokana na watumishi hewa bungeni. Hii imechangiwa na mfumo wa kutia dole (Finger print) kutofanya kazi.

Ameliomba bunge kurudisha mfumo wa wabunge kusaini kwenye makaratasi mpaka hapo baadae mfumo wa utambuzi wa alama za vidole utakapokaa vizuri ili kuokoa pesa za walipa kodi.
 
Nilimsikia sana lakini nadhani hata spika anastahili aelewe mchango wa mbunge isiwe ni kukaa bungeni tu. Wanaokaa ndani na kutozungumza lolote hadi mwisho hawana maana kabisa! Wanaosinzia nao ni hovyo tu! Kwa nini ulipe watu wanaosinzia bungeni?

Leo hii kila wakati viti viko tupu na unaweza kufika pale VETA ukakuta mbunge anakata kinywaji saa 5.
 
Mmmmmh, watumishi hewa? Yaani Magufuli anapambana na watumishi hewa ofisi na taasisi za umma, wanafunzi hewa, kumbe hata bungeni kuna wafanyakazi hewa? Uongozi wa bunge tafadhali toeni ufafanunuzi, sisi huku EFD's hazitoze ktk faida, zinatoza ktk mauzo!
 
WABUNGE HEWA, WANAKUJA SIKU YA USAHILI , SIKU NYINGINE HAWAPO.

NCHI HII KILA KITU HEWA,
TUNA SAFARI NDEFU
 
Bunge mbona limeshapoteza mabilioni kwa miaka mingi kwa kuwa na wabunge washangiliaji na mabubu!
 
Yeye mwenyewe hewa, hana hata hoja za msingi amekazana na ubaguzi tuu, sijui ndio tatizo la jimbo lake?!
 
hili bunge linachukua mda mrefu bila sababu,, bunge la bajeti lingechukua mwezi mmoja inatosha maana sioni hata wabunge wanachobadili kwenye bajeti za wizara mbalimbali. Badala ya wabunge kujikiti kwenye bajeti husika na kuhoji matumizi ya mafungu mbalimbali ya wizara utasikia kwangu hakuna maji, hakuna barabara, hakuna hospitali,,,,
 
Umechangia bungeni mara zero lakini kila siku uko bungeni na aliye changia mara 20 siku asipo ingia bungeni ni nani hewa sasa....
 
Filikunjombe alisema kuna wabunge wanakaa mwaka mzima hawajaongea kitu eti kwa vile ukikaa kimya unapewa uwaziri.
 
Anataka Kumaanisha kwamba kumbe wabunge wanalipwa kwa kuhudhuria na kusema ndioooo, yani ukiwepo mle na kupiga usingizi basi ruksa
 
Huyu kesi anapendwa sana na ccm maana siku zote yeye kazi yake ni kumsifia Raisi na Mwenyekiti wa ccm, ila ni mropokaji sana, nahisi kuna kitu kinakosekana kwenye kichwa chake
 
Hao ndiyo Wabunge hewa badala ya kutetea maslahi ya Watanzania waliowachagua ili kuibana Serikali katika maovu yake na sera za kukurupuka wako busy kuhakikisha wanalinda maslahi yao chama chao cha mafisadi na jipu uchungu Tulia.

Anataka Kumaanisha kwamba kumbe wabunge wanalipwa kwa kuhudhuria na kusema ndioooo, yani ukiwepo mle na kupiga usingizi basi ruksa
 
Yaani nchii hii kweli tunakoelekea hata hatujui. Naomba tu Mungu atusaidie.
 
Back
Top Bottom