GE2025 Ally Hapi: Siku 100 za Rais Samia Zitamaliza Changamoto za Bima ya Afya

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Ally Hapi, leo Septemba 27 katika mahojiano ya Cafe Talk Jijini Dar es salaam, akijibu swali lililoulizwa na Mwaandishi wa Habari Charles William, amesema utekelezaji wa mpango wa Bima ya Afya kwa Wote utasaidia kuondoa changamoto zinazowakabili Wananchi katika kupata huduma za matibabu ikiwemo gharama kubwa za tiba na mapungufu ya vifurushi vya Bima vilivyopo sasa.

Hapi amesema changamoto hizo zitapatiwa suluhisho na kwamba mpango huo unalenga kufanikisha matibabu ya magonjwa makubwa yanayowasumbua Watanzania wengi kama saratani, magonjwa ya moyo, figo na kisukari, ambayo gharama zake za matibabu ni kubwa mno.

“Kwa mara ya kwanza, Serikali itagharamia matibabu ya magonjwa haya makubwa, hivyo changamoto ambazo wananchi wamekuwa wakilalamikia, tutazitatua kwa asilimia mia moja kupitia mpango huu” amesema Ally Hapi.

Aidha, ameeleza kuwa mpango huu utaanza kutekelezwa kwa mageuzi yatakayofanywa ndani ya Siku 100 na Mgombea urais kupitia Chama hicho cha CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan iwapo atapata ridhaa ya kuiongoza Serikali tena baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025


Your browser is not able to display this video.
 
Alikuwa wapi kufanya hayo miaka yake hii minne.
 
Kaka madarakani miaka minne, Sana Sana ubadhirifu ndio ukaongezeka msd na nhif, kiasi kwamba mifuko ya NHIF ukateterereka.
 
Usitudanganye mheshimiwa badili mbinu!!!!
 
"Ndani ya siku 100"
Miaka 60+ mmeshindwa matundu ya vyoo, ije kuwa siku 100 kwa afya, msifanye watu hawana akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…