Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,286
- 10,831
Mbunge wa Ubunge, Prof. Kitila Mkumbo amesema ni jambo la kawaida kwa kila awamu kutatua changamoto anazozikuta lakini huwa wanazitengeneza nyingine
Kwa awamu ya Rais Samia Suluhu, amesema ametatua changamoto ya kidiplomasia na uwekezaji. Pia hata kwenye masuala ya kisiasa kama ilivyoonekana hivi karibuni.
===
Mbunge wa Ubongo, Prof. Kitila Mkumbo ambaye ni mtaalamu na mdau wa elimu amesema elimu ya sasa inatengeneza wahitimu ambao hawawezi kutengeneza ajira na pia hawaajiriki
Aidha, elimu haitengenezi wahitimu wenye stadi za ufundi. Ametolea mfano wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam ilibidi watafutwe mafundi kutoka India.
Amesema ni muhimu kwa mwanafunzi kuwa na taaluma, maarifa ya msingi na stadi za kumfanya aishi ambazo ni stadi za Maisha kama ujasiriamali, ujuzi wa upishi nk. Ili muhitimu akikosa nafasi huko juu aweze kuishi