Aliyosema Gwajima yanafanana na Aliyosema Yusufu Makamba Miaka 10 Iliyopita.

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Nasikia Gwajima, anatafutwa na Kamanda Siro ili ahojiwe, Sikubaliani na Ushauri wa Gwajima wa Kutaka Mh. Magufuli apewe Uwenyekiti wa CCM. Lakini kwamba naafiki au la, At the End of the Day Sio Gwajima au Mimi tutaamua CCM wafanyeje na Chama Chao. Uwezo wa Kuamua bado Upo CCM.

Mengine aliyogusia Askofu Gwajima Ni Kuhusu watu Kuzunguka wakitaka sapoti ya Kumnyima Magufuli Uwenyeki, Hilo Ni kweli wakati Tu Magufuli alipopata Tiketi ya Kugombea wapo waliosema na tafuteni Rekodi Kuwa Magufuli hana Uzoefu wa Uongozii ngazi yoyote katika chama. (Alisema Msomi Mmoja ambaye Pia alikuwa akigombea)

2)Gwajima aligusia Juu ya Uozo ambao Mh. Mgufuli aliukuta Kila sehemu akitoa Mfano Flow meter ya mafuta. Makontena, Wafanyakazi hewa, Muhimbili, NK. Na hakuna asiyejua aliyekuwa Mkuu wa Serikali alikuwa ni Mh. Kikwete, Na Upo Msemo usemao, "Ndoo ya Lawama inaishia kwa Mkubwa"

3) Kwamba CCM Wapo Kila mara wanaotaka Rais asipewe Uwenyekiti, Ushahidi Huo Huu hapa, shutuma alizotoa Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM Mh. Yusufu Makamba Miaka 10 iliyopita.

Msikilize Yusufu Makamba.

4) Pia Gwajima alimshauri Magufuli atishie Nyau wakimnyima Umwenyekiti kwa Kuondoa Kinga kwa Marais, Sasa hayo Nayaona Ni Mawazo tu Kama aliyoyatoa Jenerali Ulimwengu, Mbele ya Mkapa akimtazama, Kwamba Kikwete ashitakiwe.

Haya Makeke hofu za Kutaka watu wahojiwe kwa Kutoa mawazo yao, hata kama ni mawazo usiyoyakubali? Itafanya Tanzania Iwe Jehanam soon!
Mimi Nafikiri Gwajima anabeef na CCM(I may be very wrong) Wakati ule walivyomwaandama kwa Kisingizio cha Kumtukana Kadinali Pengo, Lakini haya yanatakiwa yaishe.

Mimi Nilifikiri kama CCM wana Beef na Gwajima Kwa Kumsaidia Lowassa Kilogistic, wamwite wayamalize. Hii tabia ya Kucriminalize Kila mtu akitoa mawazo naona Tunapeleka Nchi Pabaya. Kama Mtu anaongea Pumba si Ukweli Utamfichua. Labda tu mtu ashauri watu wafanye vurugu au Uhalifu, Huyo akamatwe, Lakini Mtu ati akisema fulani ashitakiwe? Kwani itadhuru nini?

Lets stop Making Tanzania a Police State, It is Really Sad.
 
Suala siyo kusali kwa gwajima, elewa mantiki ya ujumbe, mbona ni rahisi tu, suala la usali na kile kilichoandikwa humu wapi na wapi kaka, try to be objective in your thinking, na kama huna cha kupost better you remain calm
 
Mkuu unasali kwa gwajima?
Hapana ila ni Rafiki yangu wa Karibu, siwezi kumkana ingawa Sijaona sababu ya kumfagilia Magufuli kwa Kila Jambo kama my Brother Gwajima. Na haina maana kuwa marafiki mtakubaliana kila jambo. Nimemjua Gwajima wakati akiwz anateseka kulala njaa akila mkate na maji yeye na Familia, Kanisa Pale hunters likiwa na waumini wasiozidi 20. Sio mtu mbaya ni mtu ambaye tu anachukia maonevu na mateso ya watu. Na ni mtu asiyehofu kusema mawazo yake. People are different unless they order somebody to commit crime, we need to let them be.
 
Kweli kabisa,,kama unaikosoa serikali hii ujue ni balaa,,si unaona wameamua kufungia wabunge na kutokurusha bungelive
 
CCM ile haipo tena

Kwishaaaaa,kwishaa kabisa nyang'anyang'a,ndembendembe,mlalo wa chali,kifo mendeee...
 
Nasikia Gwajima, anatafutwa na Kamanda Siro ili ahojiwe, Sikubaliani na Ushauri wa Gwajima wa Kutaka Mh. Magufuli apewe Uwenyekiti wa CCM. Lakini kwamba naafiki au la Ati the End of the Day Sio Gwajima au Mimi tutaamua CCM wafanyeje na Chama Chao.

Uwezo wa Kuamua bado Upo CCM. Mengine aliyogusia Askofu Gwajima Ni Kuhusu watu Kuzunguka wakitaka sapoti ya Kumnyima Magufuli Uwenyeki, Hilo Ni kweli wakati Tu Magufuli alipopata Tiketi ya Kugombea wapo waliosema na tafuteni Rekodi Kuwa Magufuli hana Uzoefu wa Uongozii ngazi yoyote katika chama. (Alisema Msomi Mmoja ambaye Pia alikuwa akigombea)

2)Gwajima aligusia Juu ya Uozo ambao Mh. Mgufuli aliukuta Kila sehemu akitoa Mfano Flow meter ya mafuta. Makontena, Wafanyakazi hewa, Muhimbili, NK. Na hakuna asiyejua aliyekuwa Mkuu wa Serikali alikuwa ni Mh. Kikwete, Na Upo Msemo usemao, "Ndoo ya Lawama inaishia kwa Mkubwa"

3) Kwamba CCM Wapo Kila mara wanaotaka Rais asipewe Uwenyekiti, Ushahidi Huo Huu hapa, shutuma alizotoa Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM Mh. Yusufu Makamba Miaka 10 iliyopita.

Msikilize Yusufu Makamba.

4) Pia Gwajima alimshauri Magufuli atishie Nyau wakimnyima Umwenyekiti kwa Kuondoa Kinga kwa Marais, Sasa hayo Nayaona Ni Mawazo tu Kama aliyoyatoa Jenerali Ulimwengu, Mbele ya Mkapa akimtazama, Kwamba Kikwete ashitakiwe.

Haya Makeke hofu za Kutaka watu wahojiwe kwa Kutoa mawazo yao, hata kama ni mawazo usiyoyakubali? Itafanya Tanzania Iwe Jehanam soon!
Mimi Nafikiri Gwajima anabeaf na CCM(I may be very wrong) Wakati ule walivyomwaandama kwa Kisingizio cha Kumtukana Kadinali Pengo, Lakini haya yanatakiwa yaishe.

Mimi Nilifikiri kama CCM wana Beef na Gwajima Kwa Kumsaidia Lowassa Kilogistic, wamwite wayamalize. Hii tabia ya Kucriminalize Kila mtu akitoa mawazo naona Tunapeleka Nchi Pabaya. Kama Mtu anaongea Pumba si Ukweli Utamfichua. Labda tu mtu ashauri watu wafanye vurugu au Uhalifu, Huyo akamatwe, Lakini Mtu ati akisema fulani ashitakiwe? Kwani itadhuru nini?

Lets stop Making Tanzania a Police State, It is Really Sad.

Bado sijakuelewa kabisaaaaa
 
Tena alihalalisha Ufisadi, Akasema Nanii sio Malaika na yeye, "anang'ombe zake na analima mananasi" Kwani kuwa na Ng'ombe Kunakufanya uwe mbaya? Hakuwa akizungumzia Ng'ombe hasa, sikiliza Vizuri.
 
Tena alihalalisha Ufisadi, Akasema Nanii sio Malaika na yeye, "anang'ombe zake na analima mananasi" Kwani kuwa na Ng'ombe Kunakufanya uwe mbaya? Hakuwa akizungumzia Ng'ombe hasa, sikiliza Vizuri.
Sasa mwenyewe alishakuambia Manji ni rafiki yake,kusoma haujui hata picha hauoni?
 
Back
Top Bottom