Aliyopata kuyasema Nyerere

babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
5,421
3,287
NI wajibu wa Rais kuwafukuza viongozi wanaofanya makosa makubwa na wanaokataa kuwajibika. Ni kazi yake mwenyewe. Mtu anaweza kumsaidia Rais kumnong’oneza waziri wake kujiuzulu lakini hawezi kumsaidia kumfukuza waziri wake. Hiyo ni kazi ya Rais peke yake. Asipoifanya, kosa ni lake peke yake.

Hiyo Ni Nukuu ya Baba Wa Taifa Juu Ya wajibu Wa Rais.

Tumpe Magufuli Muda wa kuisafisha Serikali maana ilifika hatua watu walilalama kuhusu kuchelewa kuwawajibisha Viongozi wazembe. Tukumbuke hata mh. Pinda aliwahi kulalama kuwa angekuwa na mamlaka makubwa angemtumbua Katibu mmoja kwa uzembe aliouonyesha Bungeni.

Tutamhukumu Magufuli baada ya Miaka 4 akishindwa kutuonyesha tofauti yake na Watangulizi wake, kwa sasa ni mapema kumlaumu.

Tanzania Ya Utii na uwajibikaji kuelekea unafuu wa Maisha Inakuja.
 
Back
Top Bottom